Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, August 23, 2013

KAMATI YA MUUNGANO YATATUA KERO 10

KERIO ZA MUUNGANO!

Written by   //  22/08/2013  //  Habari 
Na Janet Josiah wa Tanzania Daima
KAMATI ya pamoja ya kushugulikia masuala ya Muungano wa Serikali ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imefanikiwa kutatua  hoja 10 kati 19.
Hoja zilizotatuliwa ni suala la ongezeko la gharama za umeme kwa asilimia  21.7 kwa wateja wa Tanzania Bara na Zanzibar asilimia 168 ambalo kamati hiyo  imeafikiana na Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kufanyiwa marekebisho ya  viwango vya bei.
Msemaji wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Siglinda Chipungaupi, alisema juzi kuwa  pamoja na kufanyiwa marekebisho ya bei pia deni la Shirika la Umeme la Zanzibar  (Zeco) litapatiwa ufumbuzi.
Hoja nyingine zilizotatuliwa ni utekelezaji wa sheria ya Tume ya Haki za  Binadamu na Utawala Bora Zanzibar, sasa imefanyiwa marekebisho kupitia sheria ya  marekebisho ya sheria mbalimbali ‘Written Laws Miscellaneous Amendments’ namba 8  ya mwaka 2006 ambapo sasa inafanya kazi sehemu zote mbili.
Chipungaupi alisema pia hoja ya ushiriki wa Zanzibar katika Jumuiya ya Afrika  Mashariki ambapo iliwasilisha miradi ya maendeleo ya kiuchumi kwa ajili ya  kuijumuisha katika miradi ya kikanda inayotekelezwa katika jumuiya ya Afrika  Mashariki nayo ilipita.
Hoja ya mgawanyo wa mapato yatokanayo na msaada kutoka nje, alisema  mazungumzo yalifanyika baina ya SMT na SMZ yalifikia muafaka kwamba fomula ya  asilimia 4.5 itumike katika kuhakikisha kwamba SMZ inapata fungu lake.
Pamoja na hizo, hoja nyingine zilizokubaliwa ni za uvuvi katika ukanda wa  uchumi na bahari kuu, Uwezo wa Zanzibar kukopa ndani na nje ya nchi ambapo  makubaliano yaliafikiwa kwamba wizara zinazoshughulikia masuala ya fedha SMT na SMZ ziandae utaratibu na muongozo.
Hoja ambazo bado zipo katika mazungumzo ni suala la kodi ya mapato na zuio,  Utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asili, Ushirikiano wa Zanzibar na  Taasisi za Nje, ajira kwa watumishi wa Zanzibar katika taasisi za muungano na  mfuko wa maendeleo wa jimbo kwa SMZ.
Zingine ni malalamiko ya wafanyakazi kutozwa kodi mara mbili, hisa za SMZ  zilizokuwa kwenye bodi ya sarafu ya jumuiya ya Afrika Mashariki, tume ya pamoja,  usajili wa vyombo vya moto, kuimarika ushirikiano kwa masuala yasiyo ya muungano na kujenga udugu miongoni mwa Watanzania.
  1. Makame Ame 22/08/2013 at 10:24 um · 
    Mbona hii lugha iliyotumika ni ya kuvunganavungana tu? Hakuna Kinachofahamika. Nothing concrete. Si ajabu kuwa hakuna kitachofanyika. Hili ni zoezi la kutia tick tu lakini si la utendaji kidhati. WaZanzibar tuwe macho. Tukisinzia kitachezwa kitakomwe hapa. Mti na macho!
    • makame silima 23/08/2013 at 7:54 mu · 
      Hakuna jipya alikwisha sema Mzee Moyo kuwa vikao hivyi sio vya kutatua kero za Muungano ni kwenda kufanya day out ya Nyama choma na kukutana ccm Bara na Ccm Zanzibar .
      Mh Mzee Moyo alisema hawana uwezo wa kutatuwa kero za Muungano wote ni kada wa chama kimoja (ccm), na swala hili wanalichukulia kichama ni sio kimaslahi ya Wazanzibar wote.
      Ikiwa kweli wanataka kutatua kero za Muungano basi wawaingize Wazanzibar wa vyama na tasisi tafauti ,waangalie kuwa kero hazitotatuka?.
      Hili c jambo lao pekeyao ccm ni lakila Mzanzibar kujuwa hatma ya nchi yao na kizazi cha badae.
  2. Foum 22/08/2013 at 10:57 um · 
    Headline na uhalisi wa content haiendani, kama limekubaliwa si kwamba limeshatafutiwa ufuumbuzi, naona huyu msemaji wa hili gurupu la kuondosha kero anasema masuala Fulani yamekubaliwa na kwa sasa yamepelekwa kwa watendaji kutafutia ufumbuzi, hii ni contradiction, kwani walipokuja hao wanaosema hii ni kero hawakuwa na alternative kama solution? tuangalie hili suala la gesi, si tuliambiwa kama tayari limeshakubaliwa kutolewa, sasa mbona huuku ni miongoni mwa mambo tisa yaliobaki? Too little too late.
  3. Rocket 23/08/2013 at 2:41 mu · 
    Haya siyo mambo yanayoitwa kero za muungano. Kero za muungano ni Utaifa wa Zanzibar, sarafu, mambo ya nje na mengine mazito kama haya. Hayo yaliyotajwa humu ni geresha tu za kutaka kuwatia moyo Wazanzibari, lakini msimao wetu uko pale pale.
  4. Bosco 23/08/2013 at 4:19 mu · 
    Tanzania daima nalo ni gazeti la ccm? Naona hapo sijaona cha maana kilichoandikwa zaid ya propaganda. Eti znz epewe 4.5% ya misaada ya nje? Ujinga tu na hvo vikao vyao vya kula posho.
  5. Ashakh (Kiongozi) 23/08/2013 at 5:03 mu · 
    Hata namie sikioni mwandishi nini kakusudia kueleza. Shaka yangu hii taarifa isiwe ni ya miaka 10 nyuma.
    Haingii akilini sasa hivi tunazungumza hadithi nyengine ya mamlaka kamili azuke mwanga mmoja tumpe mwana aleye
    Tunataka haki kamili za Zanzibar na sio usanii.
  6. tuachiwe 23/08/2013 at 5:52 mu · 
    baada ya salamu,
    Yawezekana kuwa Khabari hii ni ya hivi sasa, au hivi karibuni.
    Kwa maoni yangu kuna uwezekano wa mambo mawili.
    Ama gazeti lilikosa cha kuandika, na likaona bora liandike chochote angalau kuwapumbaza wasomaji wake.
    Au, kama kawaida yao Watanganyika wamezowea kutufanya mayakhe. Kwa hivyo wanaandika utumbo kama huo ili kudanganya toto!
    Lakini tunasema, hatukubali isipokuwa mamlaka kamili!
    Zanzibar daimaaa
    Nawasilisha
  7. Ghalib 23/08/2013 at 6:13 mu · 
    Hakuna kero yoyote iliyotatuliwa kabisa, hayo yaliorodhesha hapo juu ni usumbufu wa muungano,mpaka sasa hakujabadilisha kitu wala twasira ya muungano.
    Utapeli tu.
  8. Wamtambwe 23/08/2013 at 6:26 mu · 
    Kukubaliwa haimaanishi kuwa imi katika utendaji. Kama mutafuatilia hotuba ya Mhe. Othman Masoud (AG) alisema kuhusu Account ya Pamoja ya Matumizi na Mapato ya mambo ya Muunga ilikubaliwa tang 1984. Lakini mpaka kwenye hotuba yake ya juzi alisema bado halijatekelezwa na sio kwa sababu ni wajinga au wameghafilika, bali wanajuwa itabidi watulipe pesa nyingi sana, tuchukulie kuanzia tangu hapo 1984 mpaka hivi sasa watulipe fidia hawawezi. Ndio maana alisema haiwezekani kuwa sasa waje wakae watwambi sasa tunaanza na hiyo miaka ya nyuma tuisahau.
    Au Tuseme hizi peza walipewa akina Chombo na tayari wamezila sasa wanadai Afukuzwe kwa kufichua siri za watu?
  9. Mtanzania1990 23/08/2013 at 8:14 mu · 
    MUUNGANO WENYEWE NDO KERO KUBWA…… UVUNJWE AU WA MKTABA TUUUU….
  10. Komamanga 23/08/2013 at 10:31 mu · 
    Kuna tetesi Mansour Yusuph Himid agoma kuihama ccm .
    Anasema mtoto akinyea kiganja hakikatwi.
    Anasema hayupo peke yake wapo wengi.
    Aliokua anayasema alikuwa anaagizwa na anasema kwa niaba ya watu wake ndani ya ccm.
    Mawazo yangu me nataka hao wengine waje juu kweupe waseme wanachokiamini. Wasimuachie the escape goat.
    Ni muda mzuri wa team ya Mansour kufunguka.
  11. Abdul 23/08/2013 at 10:34 mu · 
    yule kada wa ccm atokee hapa uwanjani na ni mzee wa kuchukwa posho basi leo ni aje kuchukuwa posho lake
    hapa ni utumbo tuu hakuna tena kitu chamaana

    Chanzo: Mzalendo

No comments :

Post a Comment