Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, August 24, 2013

Mansoor Kikaangoni Dodoma

Kamati Kuu ya CCM Taifa itakutana leo ifuatiwa na Halmashauri Kuu ambapo itakuwa kwa siku mbili. Ajenda Kuu ya Kamati Kuu itakuwa  kujadili maoni ya wana CCM juu ya rasimu ya Katiba, pia kikao hicho kitajadili hali ya kisiasa na hatma ya madiwani Bukoba na Masuala ya Utumishi. Na hapo kesho kutakuwa na sherehe fupi za kuzindua Baraza la Ushauri la Wazee wa CCM kabla ya kikao cha halmashauri. Baraza hilo linaundwa na Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wastaafu wote wa CCM Taifa.
Kamati Kuu ya CCM Taifa itakutana leo ifuatiwa na Halmashauri Kuu ambapo itakuwa kwa siku mbili. Ajenda Kuu ya Kamati Kuu itakuwa kujadili maoni ya wana CCM juu ya rasimu ya Katiba, pia kikao hicho kitajadili hali ya kisiasa na hatma ya madiwani Bukoba na Masuala ya Utumishi. Na hapo kesho kutakuwa na sherehe fupi za kuzindua Baraza la Ushauri la Wazee wa CCM kabla ya kikao cha halmashauri. Baraza hilo linaundwa na Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wastaafu wote wa CCM Taifa.
Salma Said
Hivi karibuni Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar, ilipitisha kwa sauti moja pendekezo la kumvua uanachama Mwakilishi wa jimbo la Kiembe Samaki na aliyekuwa Muweka Hazina wa chama hicho, Mansoor Yussuf Himid kutokana na msimamo wake madhubuti wa kuunga mkono kutaka mabadiliko ya mfumo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Pendekezo la Kamati Maalumu limekuja siku kadhaa baada ya baadhi ya viongozi na wanachama tofauti wa CCM Zanzibar kutaka Mansoor afukuzwe katika chama ili kukinusuru chama hicho na waliowaita wasaliti.
Kwa mara ya kwanza, tuhuma za Mansoor zilifikishwa katika kikao cha Kamati ya Maadili ya CCM Zanzibar Agosti 16, 2013 katika Ofisi za CCM Kisiwandui ambapo wajumbe wa kamati hiyo kwa kauli moja walitoka na azimio la kumfutia uanachama wake mwakilishi huyo ambaye amepata umaarufu mkubwa hivi sasa.
Lakini sio Mansoor peke yake anayeshutumiwa ndani ya chama hicho kuwa anasaliti chama, Pia aliyekuwa Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume na Muasisi wa Muungano na Mapinduzi Mzee Hassan Nassor Moyo nao wakionekana kuunga mkono hoja ya kutaka mabadiliko katika Muungano ambayo ndio yatakayoiletea Mamlaka Kamili ya Zanzibar. Huku wakishutumiwa kuwa wanaunga mkono hoja za Taasisi za Kiislamu na Uamsho.
Tetesi za kutaka kuwatimua ndani ya chama ziliazia chini kwa chini kuzungumzwa na wanachama wa kawaida wa chama na baadhi ya viongozi wakuu wakiwemo wale wanaofanya kazi ndani ya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui ambapo pamoja na mambo mengine wakiahidi ipo siku watawataja majina waliowaita wasaliti wote waliomo ndani ya chama hicho lakini siku chache baada ya kauli hiyo kuzungumzwa mitaani kile kilichoelezwa kilidhihirishwa uwanjani.
Mkutano huo wa hadhara ulioitishwa katika eneo la Magomeni uwanja wa Mabata ndio uliodhihirishwa kwa kutajwa majina watu watatu ndani ya chama akiwemo Mansoor, Eddy Riyamy na Mohammed Hashim wakitajwa kama ni watu hatari ndani ya chama cha CCM kwa kuwa wanaunga mkono vuguvugu la kutaka mabadiliko ndani ya Muungano lakini katika mkutano huo palisemwa kwamba wapo wengine wakubwa zaidi ndani ya chama hicho wapo nyuma ya pazia na itafika siku yao ya kutajwa hadharani pia.
Baadae CCM Mkoa waliitisha kikao na kujadili kwa kina suala hilo la waliowaita wasaliti wakisema wapo baadhi ya wana CCM wanabeba bango la wapinzani kutaka mfumo mpya wa Muungano ambao unajulikana kama Muuungano wa Mkataba na kutaka Mamlaka Kamili ya Zanzibar ambao umekuwa ukipigiwa debe zaidi na Katibu Mkuu wa CUF na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad.
Kando ya Maalim Seif kupigia debe Muungano wa Mkataba lakini taasisi za kiislamu Zanzibar zilizoundwa chini ya Mwamvuli wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) nazo zilikiwa na wimbo huo huo huku asilimia kubwa ya wazanzibari wakionekana  kukubaliana na mfumo huo.
Licha ya kuwa viongozi wa Taasisi za Kiislamu kusekwa ndani kwa zaidi ya miezi 18 bila ya kupewa dhamana na kesi yao kudorora (mwendo wa jongoo) lakini bado kilio chao kinaendelea kusikika katika mitaa mingi ya Zanzibar na wafuasi wao ambao mara kadhaa wanapopata majukwaa hupaza sauti zao wakisema wataendelea kudai mamlaka kamili ya Zanzibar na kukataa mfumo wanaouita kandamizi wa Muungano.
Kamati Maalumu ilikaa chini ya Mwenyekiti wake Makamo Mwenyekiti wa CCM Dk Ali Mohammed Shein ambapo baadhi ya wajumbe walikubaliana ambapo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Borafia Silima Juma alisimama na kutoa pendekezo la kutaka kufukuzwa uanachama Mansoor  kwa madai amekwenda kinyume na sera ya chama hicho kwa kushirikiana na wapinzani.
Tuhuma za Mansoor zilizowasilishwa katika Kamati Maalumu zilikuwa tatu, ikiwemo kushindwa kusimamia malengo, madhumuni na masharti ya chama, kutokusimamia wajibu wa mwanachama kwa kukiuka maadili ya kiongozi wa CCM na kwa kukiuka Ilani ya chama hicho ya mwaka 2010.
Naye Makamo Mwenyekiti wa Wazazi Zanzibar Dogo Idd Mabruk alisema umaarufu wa Mansoor kisiasa ulitokana na nguvu ya CCM na hana ubavu wa kushinda uwakilishi katika jimbo la Kiembesamaki hata akifukuzwa uanachama leo.
Dogo alisema kuwa hakuna haja ya kuendelea kumbembeleza mwanachama ambaye si mtii wa katiba ya CCM na misimamo yake na kueleza kuwa kubaki na aina ya wanachama hao ni hatari kwa uhai wa CCM.
Mtu pekee alioonekana kuwa na mawazo tofauti ni Waziri asiye na wizara maalumu, na Mwakilishi wa Chumbuni, Machano Othman Said ambaye pamoja na mambo mengine alipinga kuvuliwa uanachama wa Mansoor  peke yake kwa madai ya kuzungumzia sera ya Muungano wa Serikali tatu wakati wanachama wengine ambao wamelizungumzia suala hilo wakaachwa bila ya kuchukuliwa hatua na kushauri kuitwa kujieleza badala ya kuadhibiwa kwa kunyanganywa kadi.
Mara kadhaa katika mahojiano yake na waandishi wa habari na hata pale alipoitwa kujitetea na katika kikao cha mkoa Mansoor alisema yupo tayari kufungwa, au kunyongwa amma hilo la kufukuzwa katika chama chake lakini aliahidi kusimamia kile anachokiamini ambacho ni kufanyika mabadiliko ndani ya Muungano.
Mwakilishi huyo wa jimbo la Kiembesamaki Masoor Yusuph Himid ni mtoto wa muasisi wa Mapinduzi Zanzibar ambaye pia ni shemeji yake Rais wa awamu ya sita Dk.AMani Abeid Karume, ni miongoni mwa wanasiasa wanaotetea mamlaka kamili ya Zanzibar chini ya kamati ya maridhiano yenye wajumbe sita watatu kutoka CCM na wengine CUF.
Mansoor, ameanza kupata umaarufu mkubwa kwa Wazanzibari tokea alipoanza kuonesha msimamo wake juu ya suala la gesi na mafuta ambaye ni miongoni mwa wawakilishi waliosmamia kidete na kusema wasiwasi kwamba mafuta yabaki kwa wazanzibari wenyewe huku akikataa kuitwa Zanzibar kuwa sio nchi.
Baadae Mansoor alianza kueleza hadharani msimamo wake wa kutaka Muungano wa Mkataba pamoja na madaraka kamili ya dola ya Zanzibar msimamo ambao unaungwa mkono na wazanzibari wengi.
Hii sio mara ya kwanza kwa Chama Cha Mapinduzi kuwafukuza wanachama wao itakumbukwa kwamba Maalim Seif Sharif Hamad naye aliwahi kuitwa katika kikao kama hicho na kutakiwa kurejesha kadi ya chama hicho akidaiwa amekisaliti chama hicho kokongwe na kuazisha upinzani ndani ya CCM  ambapo baadhi ya wana CCM walimfuata Maalim Seif na kujiweka kando kwa kuanzisha upinzani ambapo hadi leo chama chao kimekuwa ni chama cha upinzani CUF kinachochuana kwa nguvu sawa na CCM.
Wazanzibiri wengi wanasubiri hatma ya Mansoor itakayotolewa huko Dodoma katika Kamati Kuu huku wakiuliza jee Mansoor atawajibishwa kwa kufukuzwa katika chama kama alivyofukuzwa Maalim Seif au atapewa onyo na chama chake? Na jee historia inataka kujirejea? wazanzibari wamepaisha masikio yao wanasubiri.

No comments :

Post a Comment