Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, August 9, 2013

Maoni ya Ally Saleh

Written by 

Ally Saleh
CHINI NI COMMENT NILOITOA KWENYE STATUS MOJA BAADA YA KUONA MJADALA WA TUKIO LA KUTIWA TINDI KALI VIJANA WA KIINGEREZA…LAKINI MCHANGIAJI MMOJA AKASEMA “ SIJUI KWA NINI TUNAWAKUMBATIA WAZANZIBARI?” “
salaam,
Baada ya kuona comments hizi nimekuwa nikijiuliza kweli zinatokana na tukio la juzi au kuna kitu cha ziada. nimejiuliza hivyo hivyo niliposoma vichwa vya magazeti karibu mengi ya dar hivi leo. lakini baada ya kuona fukutu za maoni na mrindimio wa vichwa vya habari nimegundua mambo mawili.
Kwanza ni kuwa vyombo vingi vya ndani vimekuwa swayed na taarifa za vyombo vya habari vya nje hasa uingereza kuhusu tukio hili. na kwa hivyo watanzania wenzetu wa magazeti wameandika taarifa zao kama ambavyo wazungu wametaka au they have played their tune.
Magazeti ya ulaya yameanza hata kuimba ni kwa sababu walikuwa ni WAYAHUDI. tukio moja la acid kwa mzungu limekuwa ZANZIBAR KWATISHA kwa mujibu wa Habari Leo na pia kwa JamboLeo ni UNYAMA. lakini wiki tatu tu nyuma mfanyabiashara wa HOME SHOPPING alitiwa tindi kali…na haikuwa kama hype hii ya sasa.
Ni tukio baya, ovu, lakini linaweza kutokea popote. Ni kweli motive yake imejificha kwa sababu wasichana hao hawakuibiwa. Kama ni vurugu za kidini kila pahala zipo Sheikh Ponda mmoja tu anatosha kuitikisha na ameitikisa Serikali ya ya Tanzania Bara na kadhalika vurugu za makanisa ni za kila siku mpaka kuuana.
Lakini kwa watu wengi wa Bara huona mavi ya Wazanzibari yananuka zaidi. Kwa mfano comment moja humu inasema hakuna haja ya kuwakumbatia Wazanzibari jambo ambalo limekwenda kwenye siasa na unaona kuwa hilo si straight thinking wala si reasonable thinking.
Wale wasichana walipaswa kuambiwa kuwa wakati wa futari si vyema kutembea mitaani na kuwa ni muhimu ukiwa Roma ni lazima ufuate matakwa ya Warumi na utamaduni wa Zanzibar ni lazima ulindwe. Mbona Mzungu akienda Saudi Arabia anakuwa na adabu zake? Na ndio maana kuna cultural tourism.
Kui potray Zanzibar kama yalivyofanya magazeti leo ni kuua uchumi wa Zanzibar na ku undo that it will cost billions of shillings. Is dar es salaam not safe kwa sababu mfanyabiashara ametiwa acid, au ulimboka na kibanda walitekwa hviyo dar si salama au in one week watu wawili wamepigwa riasa mchana jee dar es salam si salama?
Labda kuwe na ajenda nyengine lakini tukio la Zanzibar pamoja na ubaya wake linaweza kutokea popote. Na sisi kama ndugu tunasaidianaje. Nakukaribisheni nyote msome tomsome toleo la kwanza la Tanzania la online newspaper ( ( bado wazanzibari huwa wa mwanzo na wengine hufuatia) jina ni ZANZIBARDAIMA ONLINE, ambalo limezinduliwa leo muone maoni ya MZUNGU anaeishi zanzibar juu ya tukio hili.
Chanzo: Mzalendo


No comments :

Post a Comment