NA AHMED MAKONGO
5th August 2013
Polisi wilayani hapa wamethibitisha kutokea kwa mauaji hayo ya kutisha usiku wa kuamkia juzi katika Kijiji cha Kisangwa Kata ya Mcharo, kwenye sherehe ya ufunguzi wa nyumba ya ndugu wa wanandoa hao kijijini hapo.
Afisa Mtendaji wa Kata hiyo, Waziri Kingi alimtaja mwanamke aliyeuawa kwa kunyongwa na mumewe kuwa ni Paulina Samson Misinzo.
Kingi alisema Masanja naye aliuawa baada ya kukamatwa na wananchi hao mlimani alikokimbilia kujificha.
Inadaiwa kuwa siku ya tukio hilo Masanja aliyekuwa ametegana na mkewe kwa zaidi ya miezi miwili baada ya kutokea ugomvi wa kifamilia, alimfuata mwenza wake huyo kwenye sherehe hiyo usiku.
Inadaiwa kuwa baada ya kufika nyumbani hapo huku akiwa na watoto wao wawili, alimuita mkewe huyo aliyekuwa akicheza muziki na kumpeleka nyuma ya nyumba ambako inadaiwa alimuua kwa kumnyonga kwa kutumia mikono yake hadi kufa.
Inaendelea kudaiwa kuwa baadaye alibeba mwili wa mkewe huyo na kuutupa pembezoni mwa nyumba ya jirani. “Alifika na watoto wao wawili na kimuita mkewe na kumtoa pembeni… sasa sisi tukadhani labda anaongea naye tu huko nyuma, kumbe huko ndiko alikomnyongea, ” alidai ndugu mmoja wa wanafamilia ya wanandoa hao.
Mashuhuda wengine walidai kuwa baadaye Msanjaa alikimbilia mlimani na kukamatwa siku iliyofuata asubuhi na wananchi hao waliokusanyana kwa kupiga yowe.
Wanadai mashuhuda hao kuwa wananchi hao walimkamata Masanja baada ya kumsaka na kumshambulia kwa kipigo hadi kufa
Walidai kuwa Masanja alitengana na mkewe huyo baada ya kuchoshwa na vipigo vya mara kwa mara kila siku alipokuwa akirejea nyumbani akiwa amelewa.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment