Mungu aliyeibiwa huko Zanzibar majuzi!
Wezi Waiba Mungu wa Mabaniani.
Na Mwandishi wetu
POLISI Mkoa wa Mjini Magharibi wanawatafuta watu waliomuiba Mungu wa Mabaniani katika Jamat la Kiponda mjini Zanzibar.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam, amethibitisha tukio hilo na kusema wizi huo umefanywa mwishoni mwa wiki iliyopita.
Alisema wezi hao walimuiba Mungu huyo bila kuvunja mlango wala kufuli za Jamat hilo, hali inayothibitisha kwamba wizi huo umefanywa na miongoni mwa waumini wa Jamat hilo.
“Tunaendelea kuwatafuta wezi wa Mungu huyu lakini uchunguzi wa awali unaonesha wezi hawatoki mbali, lazima wanatoka ndani ya Jamat kwa sababu hakuna mlango wala kufuli zilizovunjwa,” alisema.
No comments :
Post a Comment