NA MWINYI SADALLAH
25th August 2013
Mpango huo umetangazwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko huo, Ladislaus Mwamanga, katika warsha ya kuwajengea uelewa wa Mpango wa kunusuru kaya masikini kwa viongozi wa mikoa, wilaya na watendaji iliyofanyika Chukwani, Zanzibar.
Alisema utafiti umebaini kuwapo kwa kaya 275,00 ambazo zinakabiliwa na umasikini mkubwa na kushindwa kumudu mahitaji muhimu kama milo mitatu kwa siku na kuduma nyingine za Jamii kama afya na elimu.
Mwamanga, alisema Mradi huo, wa miaka mitano mambo matano yatatekelezwa na TASAF, ikiwamo kuboresha maisha na kuongeza kipato kwa kaya masikini kupitia uwekaji akiba na shughuli za kiuchumi kwa wananchi wenye maisha magumu.
Alisema Tasaf itatoa ruzuku kwa kaya masikini sana ili ziweze kupata huduma ya elimu, afya pamoja na kutoa ajira wakati wa majanga kama ukame na mafuriko, visiwani humo.
Alisema kuwa Mradi huo, unatarajia kunufaisha watu milioni 1.5, kati ya milioni 13.5 ambao wanaokadiriwa kuishi katika hali ya umasikini Tanzania bara na Zanzibar.
Alisema Tasaf itakuwa ikitoa ruzuku ya Dola za Marekani tano kwa kila kaya kwa mwezi ili kuziwezesha kupata huduma za elimu na afya mbali na kuzijengea uwezo wa kufanya kazi za kujipatia kipata kaya masikini katika shehia zao Unguja na Pemba.
Mwamanga alisema kuwa Mradi huo umepanga kutumia Sh. 430 bilioni ambapo wananchi watatakiwa kuibua miradi ya maendeleo itakayosaidia kuwapatia kipato na kuimarisha upatikanaji wa huduma za jamii.
Akifungua warsha hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Abdalla Mwinyi Khamis, alisema Mradi huo, una umuhimu mkubwa katika kufanikisha mpango wa serikali wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini kwa wananchi wake.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
No comments :
Post a Comment