Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, August 24, 2013

Viongozi wa CCM wanaumizana kijinga zama hizi

Rais wa Zanzibr, Dk Mohammed Ali Shein akihutumia taifa katika kilele cha maadhimisho ya sherehe za Mapinduzi
Rais wa Zanzibr, Dk Mohammed Ali Shein akihutumia taifa katika kilele cha maadhimisho ya sherehe za Mapinduzi
Na Jabir Idrissa
LAITI kama wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wangekuwa wanazingatia ipasavyo hotuba za viongozi wao, au hata wale waliopita zama zile zilizofuatia Mapinduzi ya Januari 12, 1964, matukio mengi yanayopita zama hizi tusingeyasikia.Viongozi wale walikuwa na busara sana, walikuwa na hekima kubwa. Wakisikiliza sana na kutafakari. Wale wakiheshimu mawazo ya wenzao walio wakiwasikiliza.
Hata walipokuwa wakitoa misimamo ilikuwa ni baada ya kuwa wamesikiliza walio chini yao. Wameyapata mawazo yao.Mzee Abeid Amani Karume, kiongozi wa kwanza wa Zanzibar baada ya mapinduzi yale, na ambaye alikuja kuwa muasisi mkuu wa Muungano wa Zanzibar na Tanganyika, dola mbili zilizokuwa huru, alikuwa mtu wa kusikiliza sana walio chini yake.Alisikiliza mawazo ya viongozi wasaidizi wake, na baada ya kutafakari mawazo yao, ndipo alithubutu kutoa kauli yake iliyoashiria msimamo wake.
Ni msimamo wake kama Karume, bali pia ulikuwa ndio msimamo wake kama kiongozi wa dola.
Hivyo ndivyo ilivyokuwa. Ndivyo viongozi wa zama zile walikuwa. Kwanza wakiheshimiana na kupendana. Tena wakisikilizana na kushauriana. Viongozi wale walikuwa wakivumiliana. Ama kwa hakika zama zile viongozi walikuwa kweli kioo kwa waliokuwa wanawaongoza.Hali ile ina tofauti kubwa na iliyopo zama hizi. Viongozi tulionao leo hawaheshimiani, hawapendani wala hawasaidiani kuzalisha mawazo.
Leo viongozi wa chama hiki hawako vile walivyokuwa wa zama zile. Kila mmoja na lake.Hata wale walikuwa na misimamo iliyotofautiana, lakini wakiheshimiana kwa kila mmoja na msimamo aliouona ni mwema. Bali hakupinga msimamo tofauti kwa sababu ya kupinga tu.
Ilipobidi akipinga kwa kutoa hoja yake dhidi ya ile ya mwenzake. Na yote yakifanyika kwa amani na salama.
Bila ya kupigana au kutumia nguvu kulazimisha mawazo yake yafuatwe na kila mmoja miongoni mwa viongozi wenzako. Viongozi wale hawakupambana. Walichagua kurahisisha mafahamiano. Mzee Karume amepita. Ingekuwa mnyama
tungesema kwa vile amepita basi, kila kilichokuwa chake kimepita. Kisizingatiwe. Kisijaliwe. Kwa kuwa amepita tuamue kivyetu. Sivyo? Tungesema hivyo kama alikuwa mnyama. Alikuwa binadamu.Kwa pale alipotoa mawazo na alipotoa msimamo wake kuhusu jambo la Uhuru, kuhusu jambo la Mapinduzi, na hatimaye kuhusu jambo la Muungano, alionesha msimamo wake.
Na ndio uliokuja kuwa dira ya taifa aliloliongoza. Alifanya vile kwa mtindo wa kuisema hoja au wazo. Akisubiri mchango wa mawazo ya viongozi wasaidizi wake. Huko ndio kupima mawazo na misimamo ya walio chini yako. Mnabadilishana mawazo.
Nia ni moja tu – kwenda pamoja katika hilo mnalolijadili.Kwa hivyo kwa kuwa mzee Karume alikuwa binadamu, mawazo yake mengi yalichukuliwa kama dira zama zile. Mengi yake yameendelea kuwa dira hata kwa zama hizi. Yale aliyokuwa akiyapanga na kuyahimiza yawe yanatekelezwa, yanakumbukwa mpaka leo.Yapo mengi ndio maana baadhi ya wakati kupitia vituo vyetu vya redio na televisheni vya umma, vinayarusha yasikike.
Ni kwa sababu yalikuwa mawazo na misimamo yenye mantiki, mengine mantiki yake ingalipo mpaka leo. Ni mawazo mazima yale kwa zama zile hadi zama hizi za leo.Hebu tumchukue Mzee (si jina, bali kwa mantiki ya utu uzima wake ulioendana na jaala ya hekima na busara), Hassan Nassor Moyo ambaye yungali hai zama hizi na amekuwa akitoa kauli na maongozi kama vile alivyokuwa akiyatoa Mzee Karume.Huyu mzee bado ana nguvu kubwa. Ana nguvu ya kusema. Tena anasema kwa ufasaha kabisa.
Mzee huyu anayajua mambo ya wakati ule si kwa kuhadithiwa, kusimuliwa. Hapana. Anayajua kwa kuyashuhudia wakati yakitendeka. Anayajua kwa kuwa mengi ya mambo yale yeye alikuwa sehemu yake.Mzee Moyo alikuwa miongoni mwa mawaziri wa awali baada ya mapinduzi. Alikuwa kijana mbichi kiuongozi. Aliipata nafasi ya uongozi wa hadhi ile kwa sababu alikuwa makini. Alikuwa mtulivu. Kwa kuonekana na sifa hizo, alitumika kusaidia kujenga nchi. Akateuliwa waziri.

Akatumika chini ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Baadaye akatumika kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya dola mbili kuunganishwa.Anajua namna mzee Karume alivyounganisha dola ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na ile ya Tanganyika.
Leo anasema wazi kuwa kazi ile ilifanywa kwa usiri mkubwa na mzee Karume.Yeye na viongozi wenzake walijitahidi kutaka kushiriki lakini haikuwezekana kwa sababu mzee mwenyewe aliiweka siri kivyake. Alikuwa na sababu zake ambazo mzee Moyo anasema labda kwa wakati ule zilikuwa sawa. Hawakuwa na namna ya kufanya. Walibaki kimya ndani ya mashaka.Walimvumilia bali walijua itakuja nafasi ya kurekebisha mambo yatakapokuwa yameharibika. Nafasi hii ilichelewa kuwadia. Sasa ndo maana leo anasimama na kusema “Sisi tuliokuwa viongozi wenu wa sirikali ya mapinduzi wakati ule tulikosea. Sote tulikosea. Sasa leo ni wakati wa kurekebisha yale makosa. Mimi nasema wazi sitaki yale makosa yaendelee leo kutuumiza katika nchi yetu.
Tuyarekebishe. Ndiyo kazi ninayoifanya. Kwenu mchukuwe jukumu tushirikiane kurekebisha.Ni bahati mbaya sana viongozi wengi wa CCM wanamtafuna kisogo mzee Moyo.
Sawa huwa wanamsikiliza. Tatizo hawazingatii yale mengi anayoyasema leo. Hawayazingatii kwa maana ya kupata mafunzo. Ninyooshe lugha – wanambeza. Nitafafanua.Mzee Moyo amekuwa akizungumzia umuhimu wa kurekebisha mfumo wa Muungano. Anataka kuwe na mfumo mpya ambao hautaiumiza nchi.
Anasema mfumo uliopo tangu Muungano ulipoasisiwa, umeiumiza Zanzibar. Kwa hivyo, upo uzoefu wa kutosha kuwa nchi yetu imeumizwa kutokana na mfumo uliopo. Anasema sasa wakati ni muafaka kurekebisha hali hii mbaya. Hapo ndipo anaweka mkazo wake kwa viongozi wa zama hizi wa CCM.
Hawamuelewi.Inakera kuona kwamba kwa kuwa viongozi wa zama hizi wameamua kutojali ayasemayo kuhusu asili ya Muungano, mantiki yake kwa wakati ule na hali anayoiona kuwa inapaswa kuzingatiwa kwa mazingira ya kileo, wanaingia katika malumbano na mapambano.Hawatoi hoja.
Hawajengi nguvu kwa hoja. Asilani abadani. Wao wanaweka au kutanguliza nguvu ndipo inafuata hoja.
Wanakosea. Huku ni sawa na mtu kununua soji kabla ya kupata punda akajua soji liwe la ukubwa gani. Au kununua nguo ya mtoto hajazaliwa.Haiwezekani hiyo. Wanajidanganya na kujiingiza katika kupitwa na wakati. Kupitwa na wakati ni jambo baya. Kwanini wajiachie kwa upuuzi na ujinga? Lazima wabadilike sasa.
Huu ndio mtihani mkubwa kwa Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, bosi wao kichama kwa upande wa Zanzibar. Somo litaendelea.

No comments :

Post a Comment