Mhe. Balozi Liberata Mulaula katika picha ya pamoja
na mkurugenzi mkuu wa CRDB Bank Dkt. Charles Kimei
wakati wageni wakiingia kwenye hafla fupi iliyoandaliwa
na CRDB kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani
kwa ajili ya kutangaza huduma mpya za kibenki
kwa ajili ya Diaspora na maboresho ya huduma ya Tanzanite.
Waziri wa Fedha na Uchumi Dkt. William Mgimwa akiingia
kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani
kulikofanyika hafla fupi iliyoandaliwa na CRDB Bank
Jumatano Oct 9, 2013 kwa ajili ya kutambulisha huduma
mpya za Benki hiyo kwa ajili ya Watanzania wanaoishi nje ya nchi.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwatamburisha
waheshimiwa wageni kwa baadhi ya Watanzania
walofika kusikiliza huduma mpya za Benki ya CRDB
kwa ajili ya Diaspora na maboresho ya huduma ya
Tanzanite na baadae kumkaribisha mkurugenzi
mkuu wa CRDB Bank Dkt. Charles Kimei kuongea
na WanDMV kwa niaba ya WanaDiaspora.
Mkurugenzi mkuu wa CRDB Bank, Dkt Charles Kimei akielezea
huduma hizo mpya ambazo ni JIJENGE (Mortgage Finance)
na FAHARI HUDUMA (Argent Banking) na pia alielezea
maboresho ya hudma ya Tanzanite ikiwemo mteja
anapofkisha kiasi fulani cha pesa kwenye akaunti yake
hakutakuwa na makato ya aina yeyote yatakayokatwa kila mwezi.
Waziri wa Fedha na Uchumi Dkt. William Mgimwa
akiongea machache na kuwaambia wanaDMV
wajisikie wapo Tanzania na salama kwani
amekuja na ujumbe mzito unaowakilisha Bara
na visiwani na baadae kumshukuru Mhe. Balozi
Mulamula kwa makaribisho mazuri na CRDB Bank
kwa kuandaa hafla hiyo fupi iliyofanyikia Ubalozi wa
Tanzania nchini Marekani Jumatano Oct 9, 2013 jioni.
Waziri wa Fedha na Uchumi akiongoza ujumbe
wake kwenye chakula cha jioni.
Duputy Governor Economic & Financial Policies
Dkt. Natu El- maamry Mwamba akijiatia chakula cha jioni.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula nae akijipatia chakula cha jioni.
Kulia ni Waziri wa Fedha na Uchumi Zanzaibar Mhe. Yussuf Mzee akibadilishana mawili matatu toka kushoto ni Mariam
Mkama, Love Maganga na Tully Esther Mwambapa
ambaye nia Director of Marketing, Reserch and
Customer Service wa CRDB Bank.
Mkurugenzi mkuu wa TRA Harry Kitilya (kati)
akibadilishana mawili matatu na Mwambata
wa Jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani
Colonel Adolph Mutta (kushoto) na Afisa
Ubalozi Dkt. Switebert Mkama.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
Mshereheshaji Afisa Ubalozi Suleiman Saleh
Juu na chini wadau wakifuatilia mawili matatu
kutoka kwa watoa hutuba.
Wageni waheshimiwa wakipata chakula cha jioni.
Juu na chini ni Warizi wa Fedha na Uchumi na
ujumbe wake wakibadilishana mawili matatu
na Balozi Liberata Mulamula baada ya
kumaliza kupata chakula cha jioni kwenye
hafla fupi iliyoandaliwa na CRDB Bank
kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani akiwaaga wageni
wake mara lipomalizika hafla hiyo picha
Mhe. Liberata Mulamula akiagana na Gavana
wa Bank Of Tanzania Prof. Beno. Ndulu
kushoto ni Baraka Munisi ambaye ni
Mortgage Finance Specialist.
Baraka Munisi (kushoto akiongea jambo
na Prof Benno Ndulu huku Baraka Daudi(kati) ski sikiliza.
No comments :
Post a Comment