AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, October 17, 2013

Pinda aipongeza Benki ya Wanawake

NA MWANDISHI WETU

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amesifu jitihada za Benki ya Wanawake  Tanzania (TWB) za kutoa mikopo kwa wajasiriamali wadogo kwa riba na masharti nafuu.

Aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati akizundua tawi la benki hiyo la Mjasiriamali maeneo ya Kariakoo,  ambapo pia alizundua telephone banking na kufungua akaunti yake kwenye tawi hilo.

Pinda alisema anaridhishwa na mwenendo wa Benki ya Wanawake hasa suala la urejeshwaji wa mikopo ambapo asilimia 86 ya mikopo yote imerejeshwa.

Alitoa wito kwa wateja wote wa benki hiyo kuitumia vizuri fursa hiyo na wale wanaotarajia kujiunga wafanye haraka kwa sababu masharti ya kujiunga ni nafuu na utaratibu wa utoaji mikopo hasa kwa wajasiriamali ni wa haraka na kwa riba ndogo.

 “Hii benki kweli ni benki ya watu, maana mnakopesha kwa riba ndogo kuliko benki zingine zote, na hawa wajasiriamali mkiwawekea riba kubwa hawawezi kuja maana hawataweza kulipa, fanyeni jitihada mwende hadi vijijini hata kule kwetu Mpanda tunawahitaji sana,” alisema Pinda.

Kwa upande wake, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto aliwahimiza Watanzania kujiunga na benki hiyo ili waweze kunufaika na fursa zinazopatikana.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment