Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, November 28, 2013

BALOZI PETER KALLAGHE AITEMBELEA MERU SERVICES LTD

Tanzanians in UK!

Eneo la Canary wharf london ambalo Balozi Peter Kallaghe alifanya  
ziara ya kutembelea kampuni ya Kitanzania, Meru Services LTD. 

Tarehe 23 Novemba 2013, Balozi wa Tanzania 
nchini Uingereza, 
Peter Kallaghe alifanya ziara ya kutembelea 
kampuni ya 
Meru Services inayomilikiwa na watanzania 
waishio jijini London, 
Uingereza.
Katika ziara hiyo iliyofanyika katika kitovu 
cha sekta ya biashara 
na fedha nchini Uingereza, Canary Wharf , 
Balozi Kallaghe alijionea 
huduma zinazotolewa  na kampuni hiyo katika 
Benki ya Kimataifa 
ya Credit Suisse. Pia alikutana na kuzungumza 
na baadhi ya 
watanzania wanaofanya kazi za aina 
mbalimbali za kuhudumia Benki hiyo.

Mkurugenzi na mmiliki wa kampuni ya Meru Services LTD, Bw. Dullah Meru 
akiongea machache na balozi Peter Kallaghe
Balozi Kallaghe alifurahishwa na taarifa aliyopewa 
kuwa kampuni hiyo imekuwa ikitoa huduma 
katika Benki ya Credit Suisse kwa bidii,
ujuzi na uaminifu mkubwa 
kwa takriban miaka 15. Aidha imekuwa ikitoa 
fursa za ajira kwa makundi mbalimbali ya 
watanzania wakiwemo 
wanafunzi waishio jijini London.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Axis Europe PLC Bw Dean Richards 
akimuelezea balozi Kallaghe Umuhimu kuwepo kwa kampuni ya 
Meru Servives katika eneo hilo la canary wharf.
Katika nasaha zake, Balozi Kallaghe aliitaka 
kampuni ya 
Meru Services kutambua kuwa kuaminika 
kufanya kazi katika kitovu cha sekta ya biashara 
na fedha nchini Uingereza si jambo 
dogo na kuisihi kampuni hiyo iendelee kuitunza 
heshima hiyo kwa niaba ya watanzania wote. 

Balozi pia alitoa changamoto kwa  kampuni 
hiyo na watanzania waishio nchini Uingereza 
kutumia ujuzi na uzoefu wanaopata ughaibuni 
kama mtaji wa kuwekeza katika sekta ya huduma 
inayozidi kukuwa nchini Tanzania.

Balozi alihitimisha ziara yake kwa kuahidi 
kuwa ataendelea kushirikiana na kampuni za 
kitanzania na vijana wa kitanzania wanaoishi 
Uingereza katika kuwaunganisha na fursa 
za kiuchumi zinazojitokeza 
nchini Tanzania wakati huu.

Balozi Kallaghe na Afisa ubalozi Allen Kuzilwa wakifuatila 
jambo kutoka kwa Dean
Ahmed na Dullah Meru Mkurugenzi mmiliki wa 
Meru Services LTD wakisikiliza kwa makini
Said Surur akimuelezea Balozi jambo wakati wa mkutano 
pembeni yake kulia ni Allen Kuzilwa Afisa Ubalozi
Balozi katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanayakzi 
wa Meru Services Ltd

PICHANI CHINI NI BAADHI YA KAZI ZINAZOFANYA 
NA MERU SERVICES LTD. NA  ZILIZO KAMILIKA






Mgahawa wa wafanyakazi uliofanyiwa ukarabati na 
kampuni ya Meru Services 



Vijana wakiwa kazini kuweka nafasi ya kwa 
ajili ya wafanyakazi wapya 210 wanao hamia 
Credit Suisse London. 

Huu ndo muonekano baada ya kazi kukamilika .

Picha za kushoto ni kabla ya ukarabati 
na kulia ni baada ya ukarabati

Picha za kushoto ni kabla ya ukarabati na 
kulia ni baada ya ukarabati

Picha za kushoto ni kabla ya ukarabati 
na kulia ni baada ya ukarabati
Chanzo: SwahiliVilla
http://swahilivilla.blogspot.ie/2013/11/balozi-peter-kallaghe-aitembelea-meru.html

No comments :

Post a Comment