zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, November 3, 2013

CUF kuanza uchaguzi wa viongozi

NA BEATRICE SHAYO

3rd November 2013


Chama cha Wananchi (CUF) kimeanza mchakato wa uchaguzi wa viongozi ndani ya chama hicho ili kupata viongozi makini watakaoleta mapinduzi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi CUF, Shaweji Mketo, wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na fomu za kugombea uchaguzi wa viongozi wa chama zilizoanza kutolewa.
Alisema kuwa wanachama wameanza kuchukua fomu kuanzia jana kwa ajili ya kugombea nafasi zilizopo kwani kwa mujibu wa kanuni kila baada ya miaka mitano viongozi waliopo madarakani wakimaliza muda wao huchaguliwa wengine.
Mketo alisema uchaguzi huo umelenga kutengeneza safu imara kwa ajili ya kujiandaa na chaguzi za serikali za mtaa ambao unatarajia kufanyika mwaka 2014 pamoja na uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Alisema wanatarajia kupata viongozi wenye sifa kwa lengo la kutengeneza mikakati ya ushindi katika Uchaguzi Mkuu na lengo ni kutokuwa sehemu ya Serikali ya Zanzibar.
Mketo alisema wanataka kuichukua serikali ya Zanzibar pamoja na ya Tanzania ili waiongoze na kwamba katika hilo wamejipanga na ndio maana wanatarajia kupata viongozi makini katika uchaguzi huo.
Alisema kwa viongozi ambao wamemaliza muda wao ni kwamba wanaruhusiwa kugombea kwa mujibu wa ibara ya 103 (3) na kwamba atachaguliwa na wanachama kutokana na yale aliyoyafanya kwa kipindi alichokuwa madarakani.
Aidha, alisema nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba ipo wazi kwa yeyote anayeitaka anaweza kugombea pamoja na nafasi nyingine, hivyo wanachama waanze kuchukua fomu mapema na mwisho wa kuchukua fomu ni Novemba 10 mwaka huu.
Mketo alisema wanaanda barua kwa ajili ya kumpelekea Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi ili kumueleza kile wanachokusudia kukifanya.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments :

Post a Comment