NA MOSHI LUSONZO
30th November 2013.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana wakati akizindua tovuti kuu ya Taifa, Pinda alisema kituo hicho kitajenga mfumo imara wa kurahisisha utendaji wa serikali na upatikanaji wa huduma kwa wananchi.
Alisema kwa kutumia vijana wa hapa nchini waliosomea fani ya teknohama, wamefanikiwa kuanzisha tovuti hiyo yenye ubora unaokubalika.
"Tuwatunze vijana hawa kwa sababu wamesaidia nchi kuwa ya kisasa inayokwenda na wakati, kwa sababu watu kutoka vijijni wanaotaka kupata taarifa mbalimbali ya kiserikali hawahitaji kuja Dar es Salaam, badala yake wanapata pale pale walipo," alisema Pinda.
Waziri Pinda, alisema serikali itaimarisha kiutendaji Wakala wa serikali mtandao, iliyo chini ya Ofisi ya Rais, menejimenti na Utumishi wa Umma inayosimamia tovuti hiyo.
Aidha, alisema serikali imekamilisha kazi ya utandazaji wa mkongo wa Taifa wa mawasiliano kwa ngazi ya mkoa na wilaya na kwamba hatua iliyobaki ni kusambaza katika ngazi ya serikali za mitaa.
Pamoja na mkongo huo kupunguza gharama ya mawasiliano, bado idadi ya watu waliojiunga ni ndogo, hivyo alihimiza kuchangamkia huduma hiyo.
"Naomba vyuo vikuu, taasisi za serikali, watu binafsi na kampuni kujiunga katika mkongo wa taifa ili kupunguza gharama ya mawasiliano," alisisitiza.
Kwa upande wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa serikali mtandao (eGa), Dk. Jabir Idrisa, tovuti kuu ya Taifa itasaidia nchi kiuchumi kutokana na kutumiwa na wananchi wote katika kupata huduma.
Alisema ndani ya tovuti hiyo wananchi watapata taarifa zote za kiserikali kama uhamiaji, taarifa ya vizazi na vifo, biashara, taarifa za mambo ya nje, uwekezaji na wananchi.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment