Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, December 10, 2013

Mrema agawana mshahara na wapigakura jimboni

NA MWANDISHI WETU

10th December 2013


Mbunge wa Vunjo,Agustine Mrema ( TLP)
Mbunge wa Vunjo, Agustine Mrema ( TLP), amesema  ameamua kugawana mshahara wake na wananchi wa Vunjo kwa kuwapa mitaji ya biashara  kinamama na vijana wa jimbo hilo ili kuendeleza biashara zao na watamrejeshea baada ya nwaka mmoja.

Mrema aliyasema hayo wilayani Moshi wakati akigawa fedha kwenye vikundi vya wajasiriamali na kusema amekuwa akifanya hivyo kila  mwaka, lakini wananchi wanamwangusha na kwamba mwaka jana  alitoa Sh, milioni 25, lakini zimerudi Sh. milioni tisa tu.

Mrema alisema ameamua kuwa anafanya hivyo baada ya kugundua Watanzania wengi wanakabiliwa na changamoto ya mitaji ya kufanya biashara hasa wajasiriamali wa vijijini.

Vikundi vilivyo nufaika na fedha hizo ni vikundi tisa na kila kikundi kilipata Sh. milioni moja na timu ya mpira ya Kata ya Kahe Mashariki ilipewa fedha kwa ajili ya kuweka magoli ya kisasa katika uwanja uliopo kijiji cha Ghona.

Mwenyekiti wa kikundi cha vijana wa Marangu Mtoni, Harrion Kimati, alisema wanafurahia hatua zinazochukuliwa na Mrema kuhakikisha wanajikimu kwa mitaji.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment