Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, December 25, 2013

Saidia kufanikisha ujenzi wa skuli mpya ya Kengeja - Pemba

Written by   //  23/12/2013 

kengeja-2
Hamed Mazrui,
Baada ya Seriakali ya wakoloni ilipoamua kujenga skuli ya Kengeja Secondary mnamo mwaka 1922 na kutoa huduma za elimu kwa watu mbali mbali mpaka hivi sasa licha ya kufanyiwa marekebisho kadhaa mara kwa mara kwa skuli hio iliotokana na michango ya wananchi wenyewe sasa skuli hio imechoka na hakuna budi kujengwa mpya.
Sisi watu wa Kengeja kwa moyo wetu na uwezo wetu tayari tumechangishana kiasi cha milioni kumi na tano ili kujenga skuli yetu hii lakini kutokana na ugumu wa maisha hatuwezi kukamilisha ujenzi kama huu wa mamilioni ya nshilingi,hivo basi tunaomba msaada wenu wasamaria wema kwa kiasi chochote kile mulichonacho mukijua kwamba mnachokitoa ni sawa na sadakatul jaria kuna siku mntaikuta mbele ya Allah.

Tumeamua kuonesha mchoro huu wa Skuli ambayo itakuwa na jumla ya madarasa kumi pamoja na ofisi ya walimu.
Ujenzi huu unahitaji kiasi cha milioni mia moja na sitini namoja kwa hatua ya awali ili kuweza kukamilisha mpaka kukamilika kwake ingawa gharama zaidi zinaweza kuongezeka.
Ewe msomaji tunakuomba fikisha ujumbe huu kwa kila mtu na Inshallah Mwenyezimungu atakulipa kutokana na kusambaza kwako ujumbe huu.
Kwa mawasiliano zaidi jinsi ya kuelekezwa kuchangia piga nambari hii +255774848800 au +255777514444.

  • Hali halisi ya Skuli ya Kengeja!

kengeja
Mimi ni Skuli ya Kengeja Secondary nimezaliwa mnamo mwaka 1922 nimetoa elimu kwa watu wengi sana wa Kengeja na maeneo jirani kama vile Mwambe,Kiwani,Kangani kwa kipindi cha nyuma wakati wa kuanzishwa kwangu.
Kwa sasa naendelea kutoa elimu bado ingawa nimechoka sana kutokana na uchakavu wa majengo yangu, naomba msaada kwa Serikali na wasamaria wema kunifanyia alau ukarabati tu na ikiwezekana kujengwa upya.
kUTOKA: mazrui – fb
Chanzo: Mzalendo

No comments :

Post a Comment