Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, December 13, 2013

Spika Amelazimika kuahirisha Kikao kwa Dakika 15

Na Himid Choko.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho leo jioni amelazimika kuahirisha kikao cha baraza la wawakilishi kwa muda wa dakika 15 kutokana na wajumbe wengi kucherewa kufika katika kikao hicho.
Akizungumza baada ya kurejea tena katika kikao hicho Mhe Kificho amewataka wajumbe hao kuacha mara moja tabia mbaya ya utoro na ucherewaji katika vikao vya baraza .
Amesema chombo cha baraza la wawakilishi ni chombo kikubwa katika nchi hivyo kinapaswa kuwa kioo, hivyo si nyema kwa wajumbe wa baraza hilo kucherewa au kutoroka katika vikao hivyo ambayo vinaonyeshwa na kutangazwa moja kwa moja kupitia vyombo vya habari.Amesema amewaomba wawakilishi hao kutoendelea kujipa sura mbaya kwa wananchi na badala yake watekeleze ipasavyo majukumu waliyokabidhiwa na wananchi kwa faida yao na taifa kwa ujumla.
Aidha spika kificho amewaomba radhi wananchi kutokana na kitendo kilichofanywa na wawakilishi wao .
Wakati huo huo katibu wa BLW Yahya khamis Hamadi amesema Baraza la Wawakilishi limelazimika kuitisha Kikao cha Dharura cha Kamati ya Uongozi ya Baraza ili kujadili kitendo hicho cha leo.
Amesongeza kusema kwamba kitendo kilichoonyeshwa na waheshimiwa wawakilishi hao hii leo si nidhamu wala si cha haki hivyo Kamati ya uongozi ya baraza itakutana jumatau ijayo kuangalia uwezekano wa kubadilisha Kanuni ili kudhibiti nidhamu ya Baraza.
Amesema cha kusikitisha zaidi hii leo wakati mhesimiwa Spika anaakhirisha kikao hicho kwa muda hata wanadhimu wa vyama na serikali nao hawakuwemo wakati huo.
Zanzinews

No comments :

Post a Comment