Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, December 16, 2013

WB yautabiria mema uchumi wa Tanzania

NA JIMMY MFURU

16th December 2013


Benki ya Dunia (WB)
Uchumi wa Tanzania unaweza kukua kwa asilimia saba kwa mwaka katika miaka ijayo wakati mfumuko wa bei ukibakia asilimia tano kutokana na kushuka kwa bei za chakula na sera za fedha kubana.

Ripoti ya Benki ya Dunia (WB) ilisema kama ilivyokuwa miaka ya hivi karibuni, kukua kwa uchumi wa Tanzania kunaonekana kusukumwa na sekta, ambazo shughuli zake sehemu kubwa ziko katika miji, katika sekta za mawasiliano, uchukuzi, ujenzi na biashara za rejareja.

Ripoti hiyo inajenga hoja ya kuongeza uzalishaji katika kilimo na kutengeneza ajira nyingi nje ya shughuli za kilimo.

Inasisitiza kuwa mikakati kama hiyo haitoshi kumfanya kila mtu aondoke kwenye umaskini wakati uzoefu  duniani unaonyesha hata kama uzalishaji katika kilimo utaongezeka, huku familia maskini zaidi kawaida zikiachwa nyuma.

“Hii inaonyesha umuhimu wa kuwa na programu za hifadhi ya jamii zinazolenga kuwasaidia watu walio katika mazingira hatarishi zaidi,” alisema Mkurugenzi wa WB Tanzania, Uganda na Burundi, Philippe Dongier.

Ripoti ya hivi karibuni ya Hali ya Uchumi inaonyesha mafanikio ya Mfuko wa  Maendeleo ya Jamii (Tasaf).

Inaonyesha matokeo mazuri katika kushughulikia mahitaji ya kaya maskini zaidi, wazazi wanaopata kiasi kidogo cha fedha kila mwezi hutumia fedha hizo kununua chakula cha ziada na mahitaji ya elimu na afya ya watoto wao.   

 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment