Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, December 14, 2013

Zitto kuwasilisha hoja binafsi bungeni

NA JACQUELINE MOSHA

14th December 2013


Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto(Chadema)
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (Chadema), amesema anatarajia kuwasilisha maelezo binafsi kuhusu, kauli ya Mwanasheria Mkuu, Frederick Werema, aliyoitoa juzi bungeni dhidi yake ya kumuita muongo kuhusu mabilioni Uswis.

Zitto alitoa kauli hiyo siku moja baada ya Jaji Werema kudai mbele ya Bunge kuwa Serikali inashughulikia kisheria suala la mbunge huyo  kutokana na kudanganya Bunge na kamati.


Kwa mujibu wa Zitto, kwa sasa hataki kuzungumzia suala hilo, ila ukweli wote ataubainisha kwenye maelezo yake binafsi ambayo atayawasilisha wiki ijayo.
Nimeamua hili suala nilizungumzie ndani ya Bunge, kwa hiyo tayari nimewasilisha maelezo yangu kwenye Ofisi ya Bunge, na wameniambia kuwa nitapangiwa kuwasilisha maelezo hayo wiki ijayo, kila kitu nitakibainisha siku hiyo, sina zaidi,” alisema.

Wakati akitoa majumuisho ya mjadala wa taarifa zilizowasilishwa bungeni juzi, ambazo ni taarifa ya Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, Werema alisema katika suala hilo, Zitto amezidi kuwa mzito.

Werema ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya kuchunguza madai ya mabilioni hayo alisema ili kumalizia uchunguzi wa fedha hizo ameomba Spika wa Bunge kuiongezea kamati hiyo miezi sita.

Alisema maneno aliyoyasema Zitto bungeni humo hayafanani kabisa na mwenendo wake na kauli zake alizozitoa mbele ya kamati iliyoundwa na serikali kuchunguza sakata hilo.

Alisema Bunge lilitoa hadidu rejea kuchunguza na kubaini majina ya Watanzania wanaodaiwa kuwa na fedha nje kinyume cha sheria, kuchunguza kama fedha hizo ni haramu, kutambua benki ambako fedha hizo zipo na kuandaa mashtaka na kuishauri serikali.

Kutokana na hali hiyo, Werema alisema kamati ilikutana na Zitto katika ofisi zake zilizomo ndani ya Bunge na akawaambia kuwa anazotaarifa na nyaraka lakini akatoa masharti mawili.

Moja ya masharti Zitto alitaka kuhakikishiwa na Bunge kuwa hakuna mtu atakayemsonga baada ya kutoa taarifa na pia alimtaka Werema ale kiapo kwamba ikigundulika kama si kweli awe huru.

Alisema Machi 23, Zitto akaenda JKT Tanga lakini kamati ilipoenda Tanga kumfuata walishauriana kuwa amalize mafunzo na kwamba wakutane Dar es Salaam lakini hakufanya hivyo.

Alisema walikutana tena bungeni mjini Dodoma, alisema kuwa anakwenda Afrika Kusini na hivyo kushindwa kuhojiwa.

Hata hivyo, alisema Juni walichukua maelezo ya Zitto chini ya kiapo ambapo alisema hakuwa na jina wala akaunti ya Mtanzania yeyote aliyeficha fedha nje ya nchi.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment