Mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri na Uteuzi wa Naibu Waziri.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri na pia kumteuwa Naibu Waziri kama ifuatavyo-
(a) Mhe. Dkt. Sira Ubwa Mamboya ameteuliwa kuwa Waziri wa Kilimo na Maliasili akijaza nafasi ilioachwa wazi na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Suleiman Othman Nyanga.
(b) Mhe. Juma Duni Haji ameteuliwa kuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano akichukuwa nafasi ilioachwa wazi na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Rashid Seif Suleiman ambaye sasa anakuwa Waziri wa Afya.
(c) Mhe. Rashid Seif Suleiman ameteuliwa kuwa Waziri wa Afya akijaza nafasi ya Mhe. Juma Duni Haji ambaye sasa anakuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano.
(d) Mhe. Mahamoud Thabit Kombo ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Afya akijaza nafasi ilioachwa wazi na Mhe. Dkt. Sira Ubwa Mamboya ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Kilimo na Maliasili.
Na pia amefanya mabadiliko ya baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Wilaya.
Aidha, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya mabadiliko ya baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Wilaya kama ifuatavyo:-
(1). Major Mstaafu Juma Kassim Tindwa ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa Kaskazini Unguja akijaza nafasi ilioachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Bwana Pembe Juma Khamis.
(2). Bibi Mwajuma Majid Abdulla ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa Kusini, Pemba akijaza nafasi ilioachwa wazi na Major Mstaafu Juma Kassim Tindwa ambaye amehamishiwa Mkoa Kaskazini, Unguja.
(3). Bwana Omar Khamis Othman ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini, Pemba akijaza nafasi ilioachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Bwa. Dadi Faki Dadi.
(4). Bwana Ayoub Mohamed Mahmoud ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Magharibi akijaza nafasi ilioachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Bwa. Hassan Mussa Takrima.
(5). Bibi Hanuna Masoud Ibrahim ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake akijaza nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Bibi Mwanajuma Majid Abdulla ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa Kusini, Pemba. Utezi huo umeanza leo tarehe 24 Agosti 2014.
Chanzo: ZanziNews
No comments :
Post a Comment