dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, August 28, 2014

Ziara ya Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Singapore

 Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (wa tatu kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mawaziri saba wa Mambo ya Nje wa Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara wakiwa na mwenyeji wa Mkutano huo Waziri wa Mambo ya Nje wa Singapore Mhe. Kasiviswanathan Shanmugam (wa tano kutoka kushoto). 

  Mawaziri wa Mambo ya Nje wakiwa kwenye ziara kwenye mojawapo ya vyuo maalum nchini humo Institute of Technical Education ambapo Tanzania inashirikiana nacho kwenye kutoa mafunzo kwa walimu wa VETA.

 Mhe. Dkt.  Mahadhi Juma Maalim, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (kushoto) akikata utepe kufungua rasmi ofisi za Ubalozi wa Heshima za Tanzania nchini Singapore akishirikiana na Mhe. S.S. Teo, Balozi wa Heshima. Kulia ni Mhe. John Kijazi, Balozi wa Tanzania nchini India ambaye pia anaiwakilisha Tanzania nchini Singapore. 

 Mhe. Dkt.  Mahadhi Juma Maalim (wa pili kushoto), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa kwenye picha ya pamoja na Mhe. John Kijazi (wa kwanza kushoto), Balozi wa Tanzania nchini India ambaye pia anaiwakilisha Tanzania nchini Singapore, Mhe.S.S. Teo, Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Singapore na Balozi Mbelwa Kairuki, Murugenzi wa Idara ya Asia na Australasia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

 Mhe. Dkt.  Mahadhi Juma Maalim, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa kwenye mazungumzo na mwenyeji wa Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara Mhe. Kasiviswanathan Shanmugam, Waziri wa Mambo ya Nje wa Singapore. 

  Mhe. Dkt.  Mahadhi Juma Maalim (wa pili kushoto), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa kwenye picha ya pamoja na Mhe. Kasiviswanathan Shanmugam, Waziri wa Mambo ya Nje wa Singapore (wa tatu kushoto), Balozi Mbelwa Kairuki na Mhe. John Kijazi, Balozi wa Tanzania nchini India na Singapore.  

 wakiwa katika maongezi.

Chanzo: Vijimambo

No comments :

Post a Comment