Mkamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitia saini kitabu
cha wageni mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Chuo Kikuu Huria cha
Tanzania yaliyopo Bungo Kibaha Mkoa wa Pwani kwa ajili ya mahfali ya 26
ya chuo hicho.Aliyesimama ni Mkuu wa Chuio Kikuu Huria cha Tanzania ambae pia ni Waziri wa Katiba na Sheria Tanzania Dr. Asha – Rose Migiro.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar akiwa na Mwenyeji wake Mkuu wa Chuo Kikuu
Huria cha Tanzania Dr. Asha-Rose Migiro wakiliongoza Gwaride kulingia
kwenye uwanja wa Mahafali ya 26 ya chuo kikuu huria cha Tanzania
yaliyofanyika Makamu Makuu yake Bungo Kibaha, Mkoa wa Pwani.
Balozi
Seif akisalimiana na baadhi ya wahitimu wa shahada, stashahada na vyeti
wa chuo Kikuu huria cha Tanzania ambao wametokea Zanzibar .
Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif wa pili kutopka kulia wakiokaa akiwa katika picha
ya pamoja na Wahitimu wa Chuo Kikuu huria cha Tanzania waliosimama nyuma
pamoja na Uongozi wa Chuo hicho.
Waliosimama wa pili kutoka kulia ni Mbunge wa Jimbo la Dole Muhitimu Mh. Silvester Mabunda. Kushoto
ya Balozi Seif ni Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
Profesa Samuel Wangwe, kulia ya Balozi ni Mkuu wa Chuo ambae pia ni
Waziri wa Katiba na Sheria Dr. Asha-Rose Migiro na Makamu Mkuu wa bChuo
hicho Profesa Tolly Mbwette.(Picha na Hassan Issa OMPR)
Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewahimiza Watanzania kuitumia fursa
inayotolewa na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania { CKHT } katika
kujipatia Taaluma huku wakiendelea na shughuli zao za kazi,ajira
binafsi au kifamilia kama kawaida.
Alisema wakati chuo hicho cha
umma kinapotoa nafasi nzuri zaidi kwa Watanzania kupanua wigo wao wa
elimu ya juu ni vizuri kwa wananchi kuitumia nafasi hiyo mapema bila ya
kufanya ajizi.
Balozi Seif alieleza hayo wakati
akizungumza na walimu na wahitimu wa Vyeti, Stashahada na Shahada wa
Mahfali ya 26 ya chuo Kikuu Huria cha Tanzania { CKHT }yaliyofanyika
huko Bungo Kibaha Mkoa wa Pwani.
Alisema wanafunzi wengi wasio na uwezo wa kulipia ada katika vyuo vya mabweni wanaweza kukaa kwa muda mrefu kupata elimu hiyo endapo wataamua kusubiri Serikali au mashirika ya dini na watu binafsi kujenga vyuo na mabweni hayo.
Alisema wanafunzi wengi wasio na uwezo wa kulipia ada katika vyuo vya mabweni wanaweza kukaa kwa muda mrefu kupata elimu hiyo endapo wataamua kusubiri Serikali au mashirika ya dini na watu binafsi kujenga vyuo na mabweni hayo.
Balozi Seif alisisitiza kwamba
njia pekee ya Taifa kutaka wananchi wake wajikomboe kimaisha kutokana
na ujinga, maradhi na umaskini ni kuwawezesha kupata elimu ya juu iliyo
bora na yenye gharama nafuuu popote pale walipo katika eneo la Jamuhuri
ya Muungano wa Tanzania.
Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar alitoa mfano wa uendeshaji wa Serikali za Mitaa unavyoimarika
kila siku kutokana na wafanyakazi wengi kuhitimu elimu ya juu kupitia
mfumo uliowekwa na chuo kikuu huria cha Tanzania.
Alisema mifumo mengine ya elimu
inahitaji mwanafunzi kukaa darasani, ama kuacha kazi na wakati mwengine
kuwa mbali na familia yake kwa muda mrefu wakati uwezo wa kufanya hayo
upo kwa kutumia chuo hicho Kikuu huria cha Tanzania.
“ Kama kiongozi wa Kitaifa,
mimi mwenyewe ni shuhuda mkubwa wa jinsi ambavyo tumejionea shughuli za
uendeshaji wa Serikali za Mitaa unavyoimarika siku hadi siku kutokana na
wafanyakazi wengi ambao wanahitimu chuoni hapa ”. Alisema Balozi Seif.
Aliupongeza Uongozi wa Chuo
Kikuu Huria cha Tanzania kwa mchango wake mkubwa wa kuwainua wanyonge
wenye fani tofauti hapa nchini ambazo zinahitajika katika maendeleo ya
Taifa.
Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar aliuahidi Uongozi wa Chuo hicho kwamba Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar inaunga mkono nia ya chuo hicho ya kuanzisha Chuo Kikuu
kishiriki kipindi kufupi kijacho ili kufikia dira ya 2015 -2025 ya chuo
ilivyolenga.
Alisema juhudi za makusudi
zitawekwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikia a na
Serikali za Mikoa katika kuona eneo la ujenzi wa chuo hicho kikuu
kishiriki linapatika Visiwani Zanzibar.
Akigusia ushiriki wa wanafunzi
wanawake katika chuo hicho balozi Seif alisema idadi ya wasichana bado
ni ndogo ikionyesha takwimu ya wanafunzi 1569 mwaka 2012/2013 ikipanda
kidogo na kufikia 1668 mwaka 2013/2014 ikilinganishwa na wanafunzi
wanaume waliofikia 3107 mwaka 2013/2014 na kupanda hadi wanafunzi 3056
mwaka 2013/2014.
Balozi Seif aliwapongeza
wanawake kwa kuongeza idadi yao licha ya kwamba bado takwimu yao iko
chini. Hivyo juhudi za ziada watalazimika kuziongeza ili kujiweka tayari
katika mfumo wa Uongozi Kijinsia.
Alifahamisha kwamba hata idadi
ya watumishi wanawake katika chuo hicho bado inaonekana wachache
ikionyesha idadi ya walimu wanawake 130 kati ya walimu wote 374
ikionyesha theluthi moja tuu ya walimu hao wanawake.
“ Hivi kwa utaratibu huu hiyo
asilimia hamsini hamsini inayotarajiwa ukweli itafikiwa ? ”. Aliuliza
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Mapem,a Mwenyekiti wa Baraza la
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Profesa Samuel Wangwe alisema juhudi
mbali mbali za kuimarisha huduma za chuo zitaendelea kuchukuliwa ili
kiwe miongoni mwa vyuo vikuu maarufu Duniani.
Profesa Wangwe alisema azma ya
chuo hicho ni kuongeza idadi ya wanafunzi watakaokuwa chachu ya
ongezeko la wataalamu kitaifa na kimataifa.
Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa
Baraza la Chuo Kikuu Huria cha Tanzania alieleza kwamba zipo changamoto
zinazosumbua wana taaluma wake akizitaja baadhi yake kuwa ni pamoja na
ukosefu wa Kampuni ya uchapaji vitabu ambavyo pia hutumiwa na vyuo
vyengine vikuu pamoja na upungufu wa wafanyakazi wa taaluma kwenye
Mikoa mbali mbali hapa nchini.
Alimpongeza Waziri wa Katiba na
Sheria Tanzania Dr. Asha Rose Migiro kwa kuchaguliwa kluwa Mkuu wa Chuo
Kikuu Huria cha Tanzania.
Akitoa salamu kwa niaba ya
wawakilishi waq vyuo mbali mbali vikuu wa kitaifa na Kimataifa
Mwenyekiti wa Baraza la Elimi Afrika kutoka Nchini Zim,babwe Profesa
Primos Prasha alisema elimu huria na ya masafa ndio njia pekee
itakayolivua Bara la Afrika katika wimbi la ujinga.
Profesa Prismo ameupongeza
ushirikiano mzuri uliopo kati ya vyuo vikuu huria vya Zimbabwe na
Tanzania ambao una lengo la kusaidia jamii za Waafrika kujikomboa
kielimu.
Jumla ya wahitimu elfu 3,404
kutoka nchi mbali mbali Duniani wa fani tofauti wametunukiwa shahada,
stashahada na vyeti kwenye mahafali hayo na kukifanya chuo hicho kutoa
wasomi elfu 21,503 tokea kuanzishwa kwake mwaka 1992.
Shahada, Stashahada na vyeti
hivyo vimetolewa kutokana na fani za uzamivu ya udaktari wa falsafa,
shahada za uzamili ya sheria, shahada ya uzamili katika sheria za
teknolojia ya habari na mawasiliano.
Nyengine ni shahada ya uzamili ya elimu ya sanaa katika utalii pamoja na shahada ya uzamili ya elimu katika kiswahili.
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
kilichoanzishwa mwaka 1992 kimekuwa kikipokea wanafunzi kutoka mataifa
mbali mbali Duniani wengi wao wakitokea nchi za Jumuiya ya Afrika ya
Mashariki { EAC } pamoja na Nchi za Mashariki nas Kusini mwa Afrika {
SADC }.
Chanzo: ZanziNews
Chanzo: ZanziNews
No comments :
Post a Comment