dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, November 19, 2014

NYUMBA YA MJI MKONGWE ZANZIBAR YAANGUKA!

Moja ya Nyumba katika Mji Mkongwe Yaanguka leo asubuhi, Zanzibar.


Moja ya Jengo katika Mji Mkongwe linalomilikiwa na Ndg. Rashid Abass Imram, limeaguka leo asubuhi kutokana uchakavu wake na baadhi ya wananchi wanaokaa jirani na jengo hilo wamesema jengo hilo lilikuwa na ufa kwa muda mrefu bila kufanyiwa ukarabati na mwenye nyumba hiyo, kutokana mvua zinazonyesha hivi sasa katika visiwa vya zanzibar zimesababisha jengo hilo kupata maji nakuta zake na kuanguka.

Mashuhuda wa ajali hiyo wasema jengo hilo limepata ajali hiyo wakati wa saa moja asubuhi leo ikitokea ajali hiyo kulikuwa hakuna watu wakiwa wamekaa baraza eneo hilo hutumika kwa wakaazi wa sokomuhoga kukaa jirani na maskani ya jozcorner, Katika ajali hiyo hakuna mtu aliyejeruhiwa ila kunasemekana kuna mtoto hakuonekana mpaka sasa wanashaka kuwa labda amefunika na kivushi hicho Harakati za Kikosi cha Uokozi cha Zimamoto Zanzibar wakiendelea na kuvukua kivusi hicho kuona kama kuna mtu amefukiwa na kifusi cha nyumba hiyo
Askari swa kikosi cha Zimamoto Zanzibar wakiwa kastika jitihada za kuondoa kifusi kuangaliwa kama kuna mtu aliyefunikwa na kifusi cha jengo hilo lilioko jirani na maskani ya Joz Conern sokomumogo.  
Waokoaji wakiwa katika harakati za kuondoa kifusi kuona kama kuna mtu aliyefunikwa na kifusi hicho baada ya kuanguka kwa jengo hilo ambalo lilikuwa halina wakaazi katika jengo hilo lenye gorofa tatu kwa sasa lilikuwa halikai wati ila kulikuwa na wafanyabiashara wa vinyago milango ya chini ya jengo hilo wakati ikitokea ajali hiyo mweye duka hilo hakuwekwe katika biaashara yake.



Kutoka ZanziNews


MZALENDO.NET INARIPOTI!!!

Gorofa laanguka Mji Mkongwe

Written by  WA MZALENDO.NET
Jengo moja la gorofa laporomoka huko Zanzibar katika eneo la kihistoria Jaws Corner ndani ya manispaa ya mji mkongwe Zanzibar.
Taarifa zinasema wananchi wa karibu na eneo hilo wakishirikiana na vikosi maalumu vya serikali vinaendelea kufanya jitihada mbali mbali katika eneo hilo ikiwemo kuhakikisha hakuna athari zaidi zitakazoweza kutokea.
Baadhi ya shuhuda mmoja ameiambia mazrui media kuwa watu wana wasiwasi juu ya uwepo wa watu wawili waliokua wakipita njia hawana uhakika kama waliwahi kuvuka au laa.
Hadi sasa juhudi za kuondoa kifusi cha jengo hilo kimeanza ili kuweza kubaini kama kuna watu wowote wale waliojeruhiwa au kupoteza maisha.
Tunaendelea kufatilia kwa umakini mkubwa ili kuweza kuwapatia habari za kina na uhakika.
Endelea kuungana nasi hatu kwa hatua.
Chanzo: Mazrui Media & Communication (Facebook)
………………………………………………………………………………….
Kwa Mtazamo wangu nahisi Serikali inachangia kiasi kikubwa kutokea maafa kama haya, kwa sababu wamiliki wa nyuma wanataka kuzivunja na kujenga nyumba za kisasa, serikali inakataza kisa na sababu kivutio cha watalii, viongozi wetu wana akili nyingi sana, wanajali kuwastarehesha wazungu lakini wanapuuza usalama wa raia zao hapa ndpo CCM ilipotufikisha, mipango mibovu.







No comments :

Post a Comment