dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, November 25, 2014

TWAPIGA HARAMBE KWA NDUGU YETU SULEIMAN OTHMAN!

 

Kijana Suleiman Othuman akiwa amelazwa hospitali ya Mnazi Mmoja wodi ya chini upande wa dirisha la dawa kitanda no 12. 

 Msaada unahitajika kwa kijana Suleiman Othman Ally mwenye umri wa miaka 19, mkaazi wa Zanzibar.
Suleiman amepatwa na tatizo la uvimbe mkubwa kwenye mgongo wake baada ya kupatwa na ajali kugongwa na Vespa kwa muda wa siku nyingi tu.

Walimpeleka Hospitali ya Mnazi mmoja ambapo ilishindikana kupata matibabu kutokana na damu nyingi aliotoka wakati wa upasuaji, hivyo kuwalazimu kumshona bila ya kumfanyia operation iliyokuwa wamemkusudia.

Kijana Suleiman Othuman hali yake inazidi kudhoofika na maumivu makali alionayo kwa sasa hawezi kukaa kusimama vizuri na hata kulala inavyostahiki kwa sababu ya ule uvimbe aliokuwa nao kwenye kiuno chake kama picha inavyojionyesha.

Hivi sasa familia yake haina budi kuomba ushirikiano wa msaada wenu kwa ajili ya kumgharamia mtu mmoja wa familia kufuatana nae nchini India kwa ajili ya matibabu, kutokana na gharama ni kubwa na uwezo ni mdogo.

Hivi sasa yuko hospitali ya Mnazi Mmoja wodi ya chini upande wa dirisha la dawa kitanda no 12.

Ndugu zangu tujitahidini kuokoa maisha ya ndugu yetu Suleiman Othuman kwa hali na mali.

Kwa mtu yoyote atakayeguswa na habari hii, na mwenye kutaka kuchangia msaada wake anaweza kuwasiliana na Mama yake mkubwa. Bi Salma.

Namba yaze za simu ni-:
255777489015
Tigo: 255655489015

Pia unaweza kuwasiliana na Mdau wa Blog ya swahilivilla, Abou Shatry Number 301-278, 3977, Maryland Marekani
Email swahilivilla@gmail.com

No comments :

Post a Comment