Ng’ombe mwenye mimba akutwa amechinjwa
Ng’ombe mwenye mimba kama huyu hapa juu akutwa amechinjwa
Na Husna Sheha
NG’OMBE mmoja ambae alikuwa na
mimba ya miezi saba amekutwa amekatwa mapaja na kuchukua nyama katika eneo la
Selemu Tumbotupu wilaya ya Kaskazini ‘B’ mkoa wa kaskazini Unguja.
Ng’ombe huyo alikutwa na raia
mwema wakati akiwa anapita akielekea kondeni
kwake.
Mwandishi wa gazeti hili
alifika eneo la tukio na kumkuta ng’ombe huyo akiwa amekatwa katwa mapaja yote
manne na kuchukua nyama.
Baadhi ya wafugaji walisema
matukio ya kuchinja ng’ombe na kuondoka na nyama yamekuwa yakiripotiwa mara kwa
mara lakini hayafikishwi vituo vya polisi.
Mkuu wa kituo cha polisi
Mfenesini, Idrissa Mwazini Makame alikiri kupokea taarifa za kuuawa ng’ombe
huyo ambapo baadae alifukiwa katika tukio lililoshuhudiwa na mahakama.
Chanzo: ZanziNews
No comments :
Post a Comment