Maandamano makubwa kufanyika Zanzibar kuwalaani
wezi wa Tegeta Escrow Account!
(Zanzibar) - Habari
zilizotufikia Wana-blog wa Zanzibar Ni Kwetu sasa hivi zinaeleza kuwa kutafanyika maandamano
makubwa mjini Zanzibar katika wiki mbili zijazo ili kuwalaani wote wale
waliolipwa fedha kutoka Tegeta Escrow Account.
Nia ya maandamano
haya tunaelezwa sio kulaani kitendo hichi cha wizi tu, bali kuishinikiza serikali
ya Muungano kuwataka wote waliolipwa hizi pesa haramu kuzirudisha, pamoja na
kufukuzwa kazi kutoka serikalini na kwenye nyadhifa zozote zile, sio kwa Prof Muhongo, Maswi, Werema na Prof
Tibaijuka tu, bali pia na Waziri Mkuu Pinda, Mzee Vijisenti, Mwambalaswa, Ngeleja, pamoja na wote wale waliopokea
pesa hizi za haramu au kuzijua hizi njama za wizi kabla (Pinda). Pia, wafukuzwe kutoka kwenye chama. Chama cha CCM kisiwavumilie wezi wa mabilioni ya fedha!
Wananchi kwenye
maandamano pia wataitaka serikali ya Muungano kuichukulia hii kesi kama ni kesi
ya jinai na kwahivyo kuwachukulia hatua ya kuwapeleka kortini wote wale
waliohusika na wizi huu.
Vyanzo vyetu
vinaeleza kuwa maandamano hayatokuwa ya chama fulani bali ya Wazanzibari wote,
kwani Zanzibar Ni Kwetu imeelezwa
kwamba kuibiwa kwa serikali ya Muungano au kukosa kulipwa kodi kwa Serikali ya
Muungano ni sawa sawa na kuibiwa au kukosa kulipwa kodi kwa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, kwasababu Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inahaki ya 4.5% katika
serikali ya Muungano.
Vyanzo vyetu vya
habari vinaeleza zaidi kuwa waandamanaji pia wataitaka Serikali ya Muungano kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuifunga benki ya Mkombozi Commercial Bank na benki ya Stanbic Bank, ambazo zilisaidia katika
wizi huu.
No comments :
Post a Comment