Na Mwandishi Maalum, New York
Imeelezwa kuwa waandishi wa habari pamoja na vyombo wanavyofanyia kazi wana nafasi kubwa ya ama kuchochea uibukaji wa machafuko katika nchi zao au kuyazuia kwa kutumia kalamu zao.
Hayo yameelezwa siku ya Alhamis hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo mpya wa uchambuzi unaolenga kutathmini viashiria hatarishi vya uhalifu, mauaji ya kimbari ,uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita
Hafla ya uzinduzi wa mfumo huo ambao umeandaliwa kwa ushirikiano baina ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa kuhusu Mauaji ya kimbari na Ofisi ya Umoja wa Mataifa kuhusu wajibu wa kuwalinda raia (R2P) iliandaliwa kwa ushirikiano wa Wakilishi za Kudumu za Tanzania na Italia katika Umoja wa Mataifa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa kuhusu uzuiaji wa mauaji ya Kimbari na ulinzi wa Raia. Uzinduzi uliohudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Jan Eliasson.
Mfumo huo( framework of Analysis for Atrocity Crimes, a tool for prevention) pamoja na mambo mengine licha ya kutoa ufafanuzi, tafsri na maelezo ya kina kuhusu viashiria na mazingira ambayo yanaweza kupelekea au kusababisha mauaji ya halaiki au kimbari, uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa makosa ya kivita unapanua wigo wa kuvishirikisha vyombo vya habari na asasi za kiraia kama wadau muhimu wa si tu kufanya tathmini ya awari ya viashiria hivyo lakini ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua za mapema za kuuzia kuibuka kwa matatizo hayo katika jamii.
Mfumo huo( framework of Analysis for Atrocity Crimes, a tool for prevention) pamoja na mambo mengine licha ya kutoa ufafanuzi, tafsri na maelezo ya kina kuhusu viashiria na mazingira ambayo yanaweza kupelekea au kusababisha mauaji ya halaiki au kimbari, uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa makosa ya kivita unapanua wigo wa kuvishirikisha vyombo vya habari na asasi za kiraia kama wadau muhimu wa si tu kufanya tathmini ya awari ya viashiria hivyo lakini ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua za mapema za kuuzia kuibuka kwa matatizo hayo katika jamii.
Vyombo vya habari na Asasi za kiraia vinaelezwa kama wadau muhimu licha ya ukweli kwamba wajibu wa kwanza wa kuzuia machafuko ya aina yoyote ile pamoja na kutoa ulinzi wa raia ni wa serikali kuu.
Na kwa sababu hiyo imeshauriwa kuwa waandishi wa habari wanapashwa kwanza kutambua vyema viashiria hatarishi dhidi ya Amani na usalama na kuwa nyenzo muhimu ya kuzuia kuibuka kwa uhalifu huo badala ya kuwa sehemu ya uhalifu huo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfumo huo, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Jan Eliasson amesema , mwaka 2014 umeshuhudia umwagaji mkubwa wa damu kuliko miaka mingine yoyote.
Amesema hali hiyo inatoka na ama kwa Jumuiya ya Kimataifa kutotambua mapema na katika hatua za awali za dalili ya kutokea uhalifu na uhalifu dhidi ya binadamu au ni kwa jumuiya ya kimataifa kutofautiana kimtazamo na kimaslahi kuhusu njia muafaka za kuzuia uhalifu huo.
Akasema uzinduzi wa mfumo huo unatoa fursa kwa serikali na wadau wengine ya kutambua mapema viashiria vya uwepo wa mazingira hatarishi yanayoweza kusababisha mauaji ya kimbari, uhalifu dhidi ya binafamu na uhalifu wa kivita. Lakini kubwa na la msingi anasema ni kuzuia uhalifu huo kabla haujatokea.
Amesisisitiza kuwa uhalifu dhidi ya binadamu hauibuki mara moja, bali ni jambo linalokuwa limepangwa na kuandaliwa kwa muda mrefu ukiwashirikisha wadau mbalimbali.
Amesema hali ilivyo hivi sasa ni kwamba jumuiya ya kimataifa imejikuta ikijikita zaidi katik a kushughulikia matatizo ambayo tayari yameshajitokeza badala ya kuyazuia katika hatua za awali hali inayosabibisha kutumia gharama kubwa zaidi.
Kwa upande wake Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi, pamoja na kuelezea umuhimu na manufaa ya mfumo huo wa tathmini ya viashiria vya uwepo wa mazingira hatarishi. Amesema Tanzania inaunga mkono ushirikishwaji wa wadau mbalimbali kama sehemu muhimu katika eneo zima la Amani, usalama na ulinzi wa raia.
Hata hivyo ametahadharisha kuwa pamoja na kutambua mchango wa wadau wengine, ni vema basi pawepo na utaratibu wa uwajibikaji wa wadau hao ikiwa ni pamoja usimamizi lengo likiwa ni uwajibikani kama baadhi ya wadau hao wanakuwa chanzo au chachu cha machafuko hayo.
Aidha Balozi Mwinyi amesema Tanzania ni rafiki wa mchakato huo wa wajibu wa kuwalida raia (R2P). Lakini ni ukweli usionpingika kuwa dhana hiyo ya wajibu wa kuwalinda raia bado imegubikwa na utatamwingi na kwamba kwa nchi nyingi hususani za afrika bado dhana hiyo haijakubalika au haijapokelewa vema.
Amesema sababu ya kutopokelewa vema kwa dhana hiyo na waafrika kunatokana na ukweli kuwa dhana hiyo inalenga zaidi katika kuingilia masualaya ndani ya nchi husika na pia ni dhana inayolenga katika kuleta mabadiliko ya kiuongozi katika nchi husika ( regime change).
Na kwa sababu hiyo, Mwakilishi huyo wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa amesisitiza haja na umuhimu wa kuwapo na usimamizi na utambuzi maalumu kuhusu dhana hiyo ya wajibu wa kulinda raia bila ya kuingilia uhuru wa nchi husika.
Katika uzinduzi huo, baadhi ya wachangiaji wa mfumo huo wa thathmini pamoja na dhana ya R2P akiwamo Katibu Mkuu Msaidizi Mwandamizi anayehusika na masuala ya uzuiaji wa mauaji ya kimbari, Bw. Adama Dieng wameielezea Tanzania kama nchi ambayo ni kielelezo halisi cha Amani, usalama na utulivu ikilinganishwa na mataifa mengine Barani Afrika.
Akizungumzia wajibu wa vyombo vya habari katika kuzuia machafuko ambayo yanaweza kupelekea kutoka kwa matukio ya uhalifu na makosa ya jinai dhidi ya binadamu. Bi, Agnes kut Callamard kutoka Chuo Kikuu cha Columbia. Amesisitiza haja na umuhimu kwa waandishi wa habari kuzingatia maadili ya kazi zao huku akitilia mkazo utendaji kazi huru wa vyombo hivyo ikiwa ni pamoja na haki ya kupata habari na kusambaza habari.
Amesisitiza kuwa uzoefu umeonyesa kuwa sehemu nyingi ambapo kumetokea machafuko, vyombo vya habari vimebainika kuchangia kwa asilimia kubwa uwepo wa hali hiyo.
Naye B.i Peggy Hicks kutoka Human Rights Watch akizungumzia kuhusu nafasi ya asasi zisizo za kiserikali pamoja na mambo mengine amesema kuwa Tanzania ina mfumo mzuri unaoziwezesha asasi zisizo za kiserikali kutekeleza majukumu yao pasipo kuingiliwa sana na serikali kuu. Na kusisitiza asasi hizo za tanzania hazihitaji kujifunza kutoka nje juu ya utekelezaji wa majukumu yao.
Aidha katika uzinduzi huo Tanzania imeelezwa pia kuwa Taifa ambalo kumekuwapo na ustawi, maridhiano na kuvumiliana kwa hali ya juu baina ya madhehebu mbalimba ya dini.
No comments :
Post a Comment