
Dar es Salaam’s Mwananyamala Hospital is yet to rid itself of congestion, particularly in the paediatric ward, with anything between three and four patients sharing one bed.
With Prof Tibaijuka and Mzee Vijisenti sharing 3.2 billions between the two of them amidst the above poverty and misery in the country is a GREAT SHAME!!!
Kama ni kweli maneno ya Chief Secretary Balozi Ombeni Sefue kuwa Rais Jakaya Kikwete hawezi kuchukua hatua kwa sasa dhidi ya viongozi wanaodaiwa kuchota mabilioni ya fedha katika Akaunti ya Tegeta Escrow, hadi uchunguzi juu ya kashfa hiyo ukamilike, basi Watanzania tujue kuwa sasa tumekwisha, tena tumekwisha kabisa na nchi inakuenda na maji.
Uchunguzi huu ni kutafuta njia ya kulindana tu!
Uchunguzi huu ni kutafuta njia ya kulindana tu!
Sio hasha uchunguzi huu ukamalizikia na cabinet reshuffle.
Sote ni
lazima tuliangalie hili suala kwa upeo wa juu kabisa. Hivyo mtu anaeshutumiwa
kuua hatowekwa ndani wakati uchunguzi unafanywa na badala yake ataachiwa huru
mpaka upelelezi umalizike?
Kuua??? Ndio
kuua. Unapowaibia mabilioni ya Shilingi wananchi maskini wanaolala watu wanne kitanda kimoja hospitalini, kwa kweli hapo umeua na
hujaua mtu mmoja tu bali umeua Taifa zima. Prof Tibaijuka, Mzee Vijisenti na
wezi wengine wamewaua wananchi wa nchi hii na hukumu ya muuaji ni kifo tu.
Hivyo Prof Tibaijuka anadhani kuwa yupo mtu ambae anaweza kutoa donation ya mabilioni ya
Shilingi kwa shule ambazo zinajiendesha wenyewe na tayari zinatia faida? Mzee
Vijisenti hatuwezi kumuuliza kitu kwasababu kazowea kutuibia. Ni kweli kabisa
kuwa ukionja cha kuiba basi huwezi kuacha kuiba, sawa na yule alieonja damu ya binaadamu. Aibu ulioipata Mzee Vijisenti katika lile janga la Radar bado wewe tena ni wakujiingiza kwenye wizi mwengine?
Anyway, la muhimu
ni kuwa, safari hii Watanzania tusikubali kufanywa wajinga na wapumbavu tusiojua kitu kama huko nyuma - kwa hizi njama za wakubwa za kulindana!
Bila ya hawa wezi kufukuzwa kutoka Serikalini kwa mara moja, kulipa pesa walizozichukuwa na kufikishwa mahakamani, hukumu yetu wananchi tuje kuitoa katika mwezi wa October 2015!
No comments :
Post a Comment