dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, December 26, 2014

ZANZIBAR NI KWETU KULA KIAPU KWA MARA YA NNE CHA KUULINDA MUUNGANO!

Wasomaji wetu adhimu, 
na 
Wana-blog wote,
Kama desturi yetu, tarehe 31 December, 2014, Zanzibar Ni Kwetu (ZNP) baada ya kukutakieni kheri za mwaka mpya itakula kiapo kwa mara ya nne mfululizo, kuwa tutaendelea kuulinda Muungano pamoja na matunda yake yote kwa nguvu zetu zote za kalamu.

Suala kubwa lakujiuliza ni kuwa, Muungano gani huo ambao Zanzibar Ni Kwetu itaapa kuulinda kwa mwaka mzima ujao wa 2015?

Ni Muungano ule wa Mzee Mwanakijiji alietaka kutupa bilioni 400 (TShs) ili tutoke na tumuachie jina la Tanzania baada ya yeye kukwapuwa bilioni 306 in a day-light robbery?

Au ni Muungano ule wa wananchi ambao wameoza na wanashindwa kuanzisha African Spring (civil disobedience) ili kudai pesa zilizoporwa zirejeshwe kwenye Akaunti ya Escrow?

Au ni Muungano ule wa mtu mmoja anaeitwa Mzee Vijisenti ambae hata akiwaibia watu mchana anaogopwa hata na mkuu wa nchi kuambiwa arejeshe pesa alizopora?

Au ni Muungano ule ambao Rais wake anashindwa kuzidai zirejeshwe pesa zilizoporwa na wezi nchini, kwasababu na yeye Rais itabidi arejeshe?

Ni Muungano gani huo ambao Zanzibar Ni Kwetu itaapa kuulinda?

Tega sikio!

No comments :

Post a Comment