AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, January 30, 2015

Mugabe Mwenyekiti mpya wa AU

Rais Mugabe 
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa umoja wa Afrika Au kwenye mkutano unaoendelea mjini Addis Ababa Ethiopia
Wajumbe walimteuwa Rais Mugabe mwenye umri wa miaka tisini kwa kauli moja katika mkutano huo na kumtakia mema kwenye harakati mbalimbali za kuimarisha uchumi wa bara la Afrika.
Mugabe amechukua nafasi hiyo ya Uenyekiti kuziba nafasi inayoachwa na Rais wa Afrika Kusini Nkosazana Dlamini-Zuma.
Wadadisi wa masuala ya kisiasa wametilia shaka uteuzi huo waRais Mugabe kuongoza  Zaidi ya nchi arobaini ambazi ni wanachama wa umoja huo wakieleza kuwa Mwenyekiti huyo mpya hana mahusiano mazuri mataifa ya Magharibi
Shaka hiyo dhidi ya Mugabe pia imejadiliwa na wanasiasa kuwa pengine ikiwa chachu ya maendeleo kwa Afrika kwa kujitawala yenyewe bila kutegemea nchi wafadhili.

No comments :

Post a Comment