AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, January 31, 2015

Vijana CUF wamtaka JK awaombe radhi Watanzania

Rais Jakaya Kikwete.
Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Wananchi (JUVICUF) imemtaka Rais Jakaya Kikwete,  kuwaomba radhi Watanzania, kufuatia matukio ya kudhalilishwa viongozi wa kisiasa pamoja na raia wengine kunakofanywa na Jeshi la Polisi wiki hii hapa Dar es Salaam. Kadhalika wamehoji ni kwa nini maandamano ya upinzani ni haramu wakati ya CCM siku zote yanaruhusiwa.
 
Wakizungumza katika mkutano na wanahabari jana jijini Dar es Salaam  Mwenyekiti wa JUVICUF, Hamidu Bobali, alisema Rais Kikwete ana haja ya kuomba radhi umma kwani kitendo hicho kilichotokea ni cha kiudhalilishaji .
 
Hivi karibuni huko  Mtoni Mtongani Dar es Salaam ,  polisi ilimkamata na kumpiga Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, viongozi wengine pamoja na wananchi,  kwa kile kilichodaiwa ni kukaidi amri ya kufanya maandamano yaliyozuiliwa na polisi.Bobali alisema kitendo cha kupigwa kwa viongozi hao ni cha udhalilishaji na kwamba JUVICUF imebaini hizo ni mbinu chafu zilizoandaliwa na serikali ya CCM kumdhalilisha mwenyekiti wao pamoja na viongozi wandamizi wa chama hicho.
 
“Hali hii ilionekana jinsi ilivyojiandaa kuhakikisha wanatimiza azma yao waliotumwa na watu na baadhi ya watu kuwapiga viongozi wetu kwa kutumia nguvu kupita kiasi na hata kutumia silaha ambazo sio stahiki katika harakati za kioparesheni za polisi,” alisema
 
Aliongezea kusema: “Chakusikitisha zaidi ni kauli iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,  Mathias Chikawe, imeonyesha jinsi ambayo ilikuwa ni mpango wa serikali ya CCM na kuendeleza agizo la Waziri Mkuu Mizengo Pinda alilolitoa bungeni kuwa watapigwa tu.” 
 
Alisema umoja huo umeazimia mambo mbalimbali ikiwamo kumtaka Waziri Chikawe kujiuzulu kufuatia tukio hilo pamoja na kauli yake ya uongo ambayo ameitoa juzi bungeni.
 
Pia vijana wa CUF wameitaka serikali izifute kesi zote zilizopo mahakamini zilizotokana na tukio la Januari 27 mwaka huu, siku ambayo chama hicho kinaadhimisha mauaji ya wafuasi kadhaa wa chama hicho yaliyofanyika miaka ya nyuma.
 
Bobali alisema JIVICUF imeazimia kuandaa maandamano makubwa ya kulaani vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu vinavyofanywa na serikali ya CCM kupitia  polisi.
 
Alisema watatoa taarifa za maandamano wakati wowote na kueleza  yatafanyika lini na endapo wakinyimwa kibali yatafanyika bila kuhofu.
 
Hata hivyo, alisema wanamtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu , asikubali kutumiwa na wanasiasa kwani  wananchi wanaendelea kuliona jeshi hilo kuwa limekosa watu wanaoweza kujenga hoja mbele ya umma.
 
Alisema jeshi hilo  limetoa taarifa ya kudai kuwa wamezuia maandamano hayo kutokana na kuibwa silaha katika kituo cha polisi cha Ikwiriri mkoani Rufiji zikihofiwa kuwa zipo jijini Dar es Salaam.
 
“Hivi kuibwa kwa silaha hizo kuna husiano gani na maandamano yetu wakati wao CCM wameandaa maandamano makubwa huko Songea kusherehekea miaka  38 ya kuzaliwa CCM huko Songea  hivi silaha hizo hazifiki Songea?” alihoji na kuendelea kusema
 
“Wana CCM wamesafiri kutoka  mikoa  kwa nini basi polisi wasihofu yawezekana hatari kutokea Songea ambapo wananchi wanaweza wakawa na visasi na mafisadi pamoja na wezi wa rasilimali za taifa?,” alisema
 
Wakati huo huo  wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF), wapatao 30 wameachiwa huru  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana baada ya kutimiza masharti ya dhamana.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment