Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, February 16, 2015

Benki NMB yaanza kutoa huduma kupitia MaxMalipo

National Microfinance Bank
Benki ya NMB imeanza kutoa huduma zake kupitia mawakala wa MaxMalipo inayoendelea Kigamboni jijini Dar es Salaam, Dodoma na Arusha katika hatua ya majaribio.
 
Huduma hiyo inayojulikana kama NMB Wakala, itakuwa inapatikana kwenye maduka ya kawaida yenye huduma za MaxMalipo, inategemewa kusogeza huduma za benki hiyo mpaka vijijini.
 
Hayo yalielezwa na Ofisa Habari wa NMB, Doris Kilale, wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati wa promosheni ya NMB Wakala iliyofanyika Kigamboni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 
“NMB inaleta mapinduzi ya kibenki kwa kubuni bidhaa nyingi na zenye tija zaidi kwa wateja wetu, ndiyo maana tumebuni huduma ya NMB Wakala kwa ajili ya kuwafikia Watanzania wengi zaidi kokote waliko iwe mijini au vijijini,” alisema Kilale.
 
Alifafanua kuwa ili kuhakikisha kuwa huduma hiyo inawafikia wengi,  NMB inafanya matangazo katika eneo la Kigamboni kuhamasisha wakazi wa eneo hilo wanapata elimu zaidi ya jinsi ya kutumia huduma ya NMB Wakala.
 
Alisema katika promosheni hiyo, mwananchi yeyote anaweza kufungua akaunti na kupata kadi ya ATM papo hapo.Aidha, alisema mteja anapofungua akaunti hiyo hakuna makato yoyote ya mwezi kama ilivyo benki nyingine. 
 
Alisema huduma ya kufungua akaunti hiyo maarufu kama Chap Chap, ni nafuu ambapo mteja atatakiwa kuwa na Sh.10,000 ambapo kati ya kiasi hicho, Sh. 5,000 ni gharama ya usajili na kiasi kingine kama hicho ni akiba katika akaunti ya mteja.
 
Kwa sasa NMB inafanya majaribio katika eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam ambapo kuna maduka manane yanayofanya kazi zote kama tawi la NMB kwani huduma zakutoa na kuweka fedha, kufanya manunuzi na kulipia bili mbalimbali pamoja na kuona salio la akaunti.
 
Aliwaomba wananchi kote nchini kujiunga na huduma za benki ya NMB.
 
Baadhi ya wateja wao NMB waliopata kuzungumza na NIPASHE waliushukuru uongozi wa NMB kwa kuwasogezea huduma hizi za kibenki katika makazi yao.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment