Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, February 14, 2015

JUVI-CUF yasalimu amri kwa polisi

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba.
Jumuiya ya Vijana Taifa ya Chama cha Wananchi (JUVI-CUF) jana imesalimu amri ya polisi kwa kusitisha maandamano yao ya kuitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kuongeza muda wa uboreshaji wa uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.
 
Licha ya kusitishwa kwa maandamano hayo jana polisi kupitia vikosi vya kutuliza ghasia na askari kanzu, walitanda maeneo mbali mbali jijini Dar es Salaam.
 
NIPASHE Jumamosi, ilishuhudia maeneo ya katikati ya jiji na Buguruni kukiwa na magari ya washawasha pamoja na defenda zilizosheheni askari waliokuwa na silaha zikiwemo za moto.
 
Aidha, helikopta ya polisi ilionekana ikifanya doria maeneo tofauti ya jijini ikiwa ni pamoja na ofisi za CUF zilizopo Buguruni.
 
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba, alilazimika kufika kwenye ofisi za chama hicho saa 12:00 asubuhi jana, kuisisitizia vijana hao kusitisha maandamano hayo.Profesa Lipumba alimtaarifu Kamanda Kova kuwa tayari ameshazungumza na vijana hao kuhusu kusitisha maandamano hayo.
 
Akizungumza vyombo vya habari, Profesa Lipumba alisema kuwa, polisi imezuia maandamano hayo na wao wameona hakuna sababu ya kulumbana nao.
 
“Mkiandamana pana hatari ya kupigwa kujeruhiwa na risasi maana jeshi limejipanda kutekeleza hili, Kova alinipigia simu asubuhi hii nikamwambia tumesitisha maandamano hivyo polisi wasipige watu,” alisema.
 
Aliongeza kuwa, sababu za kusitisha maandamano hayo ni kuepusha watu kupigwa na kujeruhiwa na risasi na kukamatwa.
 
Alisema kutokana na hali halisi, chama hicho kimeona hakuna sababu ya kuingiza wanachama wake katika matatizo.
 
“Hoja ya msingi ni kwamba NEC haifanyi kazi kwa uadilifu, suala la kura za maoni haliwezi kufanyika kabla ya watu wenye sifa kuandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura,” alisema.
 
Alisema Julai 9, mwaka jana NEC ilikutana na vyama vya siasa na kueleza kuwa itakuwa na vituo vya uandikishaji zaidi ya 40,000 ambapo kila kituo kitaandikisha kwa siku 14.
 
Alisema walielezwa kuwa zoezi hilo lingeanza Desemba mosi, mwaka jana lakini badala yake lilichelewa kutoana na vifaa walivyokuwa wameviagiza kuchelewa.
 
“Walianza zoezi hilo kupitia majimbo matatu ambayo ni Kawe, Kilombero na Katavi ambapo uandikishaji ulifanyika kwa siku saba tu,” alisema na kuongeza:
 
“NEC walitueleza kuwa Kata ya Kawe, Mbweni na Bunju walivuka lengo kwa kuandikisha watu 15, 123 wakati makusudio yalikuwa ni watu 14, 312, sensa ya mwaka 2012 inaonyesha waliofika umri wa miaka 18 ni zaidi ya idadi iliyoandikishwa,” alisema.
 
Profesa Lipumba alisema kuandikisha watu kwa kutumia muda wa wiki ni kuwapotezea haki baadhi ya wananchi ambao wamefikisha umri wa kupiga kura.
 
“Juvi-CUF wanasababu za msingi kuwa wiki moja haitoshi kukamilisha zoezi hili, ndiyo maana wameomba siku ziongezwe, utendaji wa NEC unatupa wasiwasi haifanyi kazi kwa uwazi mfano ni tovuti yake haina taarifa hizi za uandikishaji, “ alisema.
 
Mwenyekiti wa Juvi-CUF, Hamidu Bobali, alisema kuwa maandamano hayo hawayasitishi kwa sababu ya kauli ya Kova au vitisho vya jeshi la polisi bali kutokana na Profesa Lipumba kuwataka kufanya hivyo.
 
“Kauli ya Kova ni kama anakuja katika mapambano, polisi waache kutesa raia, Kova, IGP wajipime ili jeshi liendane na hali halisi ya sasa,” alisema.
 
Alisema tayari walishatoa taarifa kwenye matawi ya chama hivyo kuhusu kusitishwa kwa maandamano hayo hivyo hakuna eneo ambalo limekiuka.
 
Juvi-CUF ilipanga kuanza maandamano kuanzia Buguruni kupitia barabara ya Uhuru, Bibi Titi, Ali Hassan Mwinyi kupitia Serena hoteli kuelekea barabara ya Ohio kisha kutinga NEC iliyopo mkabala na Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment