dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, February 23, 2015

Mahafali ya kwanza ya chuo cha Zanzibar College of Business Education (Z.C.B.E) Pemba

 WANAFUNZI wanaohitimu masomo mbali mbali katika Chuo cha Zanzibar College of Business Education (Z.C.B.E)Kisiwani Pemba, wakiwa katika maandamano ya kuingia katika eneo la mahafali yao, ambapo Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe:Balozi Seif Ali Iddi alikuwa mgenirasmi.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

  MAKAMO wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe: Balozi Seif Ali Iddi katikati akiwa na wakuu wa Chuo cha ZCBE kisiwani Pemba, pamoja na mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba, Mhe:Mwanajuma Majid Abdalla mwenye mkoba, wakiingia katika viwanja vya mahafali ya kwanza ya chuo hicho.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

  WANANCHI mbali mbali na viongozi wa serikali wakiongozwa na Afisa Mdhamini Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Pemba,Mhe:Ali Nassor Mohamed wakimsikiliza kwa makini Balozi Sief Sharif Hamad wakati akitoa hutuba yake, katika mahafali ya kwanza ya chuo cha ZCBE kisiwani Pemba. .(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

  VIONGOZI mbali mbali wa Serikali wakiwemo maafisa wadhamini kutoka ofisi mbali mbali, maafisa Tawala na wawakilishi wa kuteuliwa, wakimsikiliza Balozi Seif Ali Iddi wakati alipokuwa akitoahutuba yake katika mahafali ya kwanza ya chuo cha ZCBE kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
  
 
MWENYEKITI wa baraza la Chuo Cha Zanzibar College Of Business Education (Z.C.B.E) kisiwani Pemba, Mhe:Hemed Suleiman Abdalla akitoa maelezo ya chuo kwa wageni mbali mbali waliohudhuria mahafali ya kwanza ya Chuo hicho.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

  MKUU wa mkoa wa kusini Pemba Mhe:Mwanajuma Majid Abdalla, akizungunza katika mahafali ya Kwanza ya chuo cha Zanzibar College Of Business Education (Z.C.B.E) kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

  WAHITIMU wa fani ya Manunuzi na Ugavi wa Chuo cha Zanzibar College Of Business Education (Z.C.B.E) kisiwani Pemba, wakivaa kofia zao baada ya kutunukiwa astashahada zao na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe:Balozi Seif Ali Iddi wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo hicho.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

  WAHITIMU wa fani mbali mbali katika chuo cha Zanzibar College Of Business Education (Z.C.B.E)Kisiwani Pemba, wakiwa na huzuni baada ya kutunukiwa astashahada zao na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe:Balozi Seif Ali Iddi wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo hicho.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

 MAKAMO wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe:Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi cheti na fedha shilingi laki mbili, mwanafunzi Mohammed Suleiman Khalfan, baada ya kuibuka mwanafunzi bora katika fani ya Uhasibu, wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo cha Z.C.B.E Kisiwani Pemb.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

Chanzo: ZanziNews

No comments :

Post a Comment