dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, February 25, 2015

TAARIFA: Andrew Chenge ni nani?

Image result for andrew chenge of tanzania

Above ni Andrew Chenge - Joka makengeza!

00000000000000000000
KWA UFUPI:Si mzungumzaji sana kwenye vikao vya Bunge na hivyo haandikwi sana na vyombo vya habari, lakini kunapotokea masuala mazito, jina lake hung’ara na wengi kujiuliza Chenge ni nani anayeweza kupita kirahisi kwenye masuala kama hayo.
Baraza la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma leo linaanza kumhoji mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge kutokana na kutajwa kwenye sakata la uchotwaji wa fedha kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow, akiwa mmoja wa watu kadhaa watakaofika kwenye Ukumbi wa Karimjee kwa mashtaka tofauti.
Si mzungumzaji sana kwenye vikao vya Bunge na hivyo haandikwi sana na vyombo vya habari, lakini kunapotokea masuala mazito, jina lake hung’ara na wengi kujiuliza Chenge ni nani anayeweza kupita kirahisi kwenye masuala kama hayo.
Mbali na sakata hilo la escrow, Chenge alitajwa pia katika kashfa ya ununuzi wa rada, ambayo ilimlazimu kuachia uwaziri.
Akiwa ni msomi aliyehitimu Shahada ya Umahiri wa Sheria kwenye Chuo Kikuu cha Harvard cha Marekani -- moja ya vyuo bora kabisa duniani-- Chenge amekuwa nadhifu katika mambo yake na ni mara chache sana waheshimiwa wabunge hujitokeza na kumtuhumu waziwazi kuhusika kwenye kashfa.
Wakati akichangia moja ya mijadala kwenye Mkutano wa 16/17 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Halima Mdee alijaribu kumtaja Chenge waziwazi kuwa anahusika katika kila mikataba yenye matatizo, lakini mwanasheria huyo wa zamani alimzima kwa kuomba mwongozo na kumtaka spika amlazimishe mbunge huyo wa Kawe awasilishe ushahidi wa anachokisema, la sivyo aache kuchafua watu.
Mdee hakuweza kuwasilisha na badala yake, akaachana na hoja hiyo na kuendelea na mambo mengine. Siku hiyo, mwanasheria huyo alionekana kuchukizwa na kwa mwonekano wa sura yake alipania kutumia umahiri wake wa kisheria kukomesha shutuma zinazorushwa kwake mara kwa mara, lakini kitendo cha Mdee kutoendelea kilimrudisha nyuma. Lakini hiyo haikuondoa ukweli kuwa Chenge alitajwa kwenye kashfa ya ununuzi wa rada ambayo ilichunguzwa na kitengo cha makosa makubwa ya jinai cha Uingereza kilichokuwa kikichunguza uamuzi wa Tanzania kununua kifaa hicho cha mawasiliano kwa bei kubwa wakati Serikali ikishindwa kutoa huduma kwa wananchi.
Rada hiyo ilinunuliwa kutoka kampuni ya BAE System ya Uingereza kwa Dola 40 milioni mwaka 2001, kiwango kilicholistua hadi Bunge la Uingereza.
Katika uchunguzi wa suala hilo, ilibainika kuwa Chenge alikuwa na akaunti kwenye kisiwa cha Jersey iliyokuwa na zaidi ya Dola 1 milioni (sawa na zaidi ya Sh1.8 bilioni kwa kiwango cha sasa).
Kinachofanya Chenge awe gumzo, ni jinsi alivyopita kirahisi kwenye kikwazo hicho. Alijiuzulu wadhifa wake wa Waziri wa Miundombinu.
Wakati kashfa hiyo imepamba moto mwaka 2008, Chenge alikuwa ziarani China akiwa na Rais Jakaya Kikwete na aliporejea aliwaambia waandishi waliomzonga kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuwa fedha hizo ni “vijisenti”. Baadaye aliitisha mkutano na waandishi wa habari na kujitetea kuwa ni muadilifu, mtu safi na hakutenda kosa katika kashfa hiyo.
Katikati ya kashfa hiyo, Chenge alihusika katika ajali iliyoua watu wawili, mmojawapo akisemekana kuwa ni mtu waliyekuwa wakifahamiana sana. Alishtakiwa kwa makosa ya kuendesha kizembe na kuendesha gari bila ya kuwa na bima. Alihukumiwa kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya Sh700,000 ambazo alilipa.
Miaka nane baadaye, Chenge alijikuta kwenye sakata la uchotwaji fedha kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow. Zaidi ya Sh306 bilioni zilichotwa na mikono ya Chenge haikuonekana hadi ulipofuatiliwa mgawo wa fedha hizo zilizotoka Benki Kuu. Ilibainika kuwa aliingiziwa Sh1.6 bilioni na aliyekuwa mmoja wa wamiliki wa IPTL, kampuni ambayo iko katikati ya kashfa hiyo.
Siku chache baada ya Bunge kumaliza kujadili kashfa hiyo na kuomba mamlaka huzika zimshughulikie yeye pamoja na wengine waliotajwa, Chenge aliibukia kwenye harambee ya majengo ya maabara ya mji wa Bariadi ambako alitoa mchango wa Sh116 milioni, kati ya Sh174 milioni zilizokuwa zikihitajika.
Kama kawaida yake, aligusia kashfa hiyo kwa maneno ya ajabu. Alisema kwa kilugha kuwa yeye ni nyoka wa makengeza na akajiita tumbiri. Hivi karibuni alikaririwa tena akisema ni nyoka wa makengeza kwa kuwa anawatafutia wananchi wake fedha.
Akiwa katikati ya kashfa ya escrow, Chenge alipewa jukumu la kuongoza Kamati ya Maandishi katika Bunge la Katiba ambalo liliondoa suala la maadili kama moja ya tunu za Taifa. Pia alishiriki vizuri katika Bunge lililojadili sakata la escrow na wakati fulani kupendekeza hata jinsi ya kushughulikia waliotajwa kabla ya mbunge wa Nyamagana, Hezekiah Wenje kuhoji sababu za mtuhumiwa kuruhusiwa kuchangia katika hoja inayomuhusu.
HISTORIA YA CHENGE
2006/15                Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti
2006/08                Waziri wa Miundombinu
2006                       Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
1993-05                Mwanasheria Mkuu
1991-93                Naibu Mwanasheria Mkuu
1972-73                Mwanasheria Mkuu
1974-75                Shahada ya Umahiri wa Sheria (Harvard)
1969-72                Shahada ya Sheria           (UDSM)
1967-98                Elimu ya Juu ya Sekondari (Mkwawa)
1963-66                Elimu ya Sekondari (St Mary’s Nyegezi)
1959-62                Elimu ya Msingi (St  Pius Minor)

No comments :

Post a Comment