Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, April 25, 2015

Wazee CUF waomba utaratibu elimu bora ya wapiga kura.

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad.
Wazee wa Chama Cha Wananchi (CUF) kisiwani Pemba, wameuomba uongozi wa chama hicho kuandaa utaratibu bora wa kutoa elimu ya wapiga kura, ili wanachama  walioandikishwa washiriki katika zoezi la upigaji kura katika uchaguzi mkuu ujao.
Wakichangia mjadala kuhusu maandalizi ya Uchaguzi Mkuu, kwenye kikao maalum cha wazee wa CUF kilichofanyika Ofisi za CUF Mkanjuni Chake Chake Pemba, wazee hao kutoka wilaya nne za Pemba, walisema ni aibu kwa baadhi ya wanachama kutoshiriki upigaji kura, jambo ambalo linachangia kukikosesha ushindi chama hicho.
Kauli hiyo waliyoitoa mbele ya Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad,  imekuja baada ya kuwapo taarifa kuwa wananchi kadhaa kisiwani Pemba hawakushiriki upigaji kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
Akichangia mjadala huo, mzee Mohammed Ali Salim kutoka Wilaya ya Mkoani, alisema elimu zaidi ya wapiga kura inahitajika ili kuhakikisha  kila aliyeandikishwa anaitumia fursa hiyo.
Walieleza haja ya kupatikana kwa vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi (ZAN ID) kwa wakati muafaka, ili waweze kuandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga kura, mwezi ujao.
Alisema baadhi ya wananchi Kisiwani Pemba  wameshajiandikisha na kupewa risiti, lakini bado hawajapatiwa vitambulisho vyao kwa  mwaka mmoja sasa. Hivyo wameiomba taasisi inayohusika kurahisisha zoezi hilo.
Akijibu hoja hizo, Mkurugenzi wa Mipango na Chaguzi wa CUF, Omar Ali Shehe, alisema chama hicho kimejiandaa kutoa elimu kwa wapiga kura ili kuhakikisha kuwa kasoro zilizojitokeza katika uchaguzi wa mwaka 2010 hazitokei tena.
Kuhusu vitambulisho, alisema licha ya kuchelewa kwa vitambulisho hivyo, lakini baadhi ya watu wameshindwa kuchukuliwa vitambulisho vyao vya kupigia kura katika ofisi za Tume ya Uchaguzi, na kuwahimiza kwenda kuvichukua.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment