Wanajumuiya ya
ZANCANA wakipata picha ya pamoja baada ya ibada ya dua maalum ya kuwaombea
walioathirika na mvua za masika, nchini Tanzania
Jumuiya ya Wazanzibari waishio nchini Canada (ZANCANA), imechangisha zaidi ya Dola 1500 za Canada kwa ajili ya waathirika wa hali ya hewa nchini Tanzania.
Katika taarifa yake ambayo Swahilivilla imeipata nakala yake, Zancana imesema kwamba mnamo tarehe 9 Mei, 2015, jumuiya hiyo iliandaa mkutano maalum wa wanachama wake katika jiji la Toronto nchini Canada.
Katika taarifa yake ambayo Swahilivilla imeipata nakala yake, Zancana imesema kwamba mnamo tarehe 9 Mei, 2015, jumuiya hiyo iliandaa mkutano maalum wa wanachama wake katika jiji la Toronto nchini Canada.
Mkusanyika huo uliofanyika katika ukumbi wa
Zancana, ulifunguliwa kwa ibada maalum ya kuwaombea na kuwakumbuka ndugu jamaa
na marafiki waliokumbwa na maafa ya hali ya hewa katika maeneo ya Pemba, Unguja
na Dar-es -Salaam.
Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa, baada ya
ibada, mawaidha na dua, kilifuatia chakula maalum kilichoandaliwa kwa ajili ya
uchangishaji wa fedha kwa lengo la kuwasaidia wahanga wa mvua za masika katika
maeneo ya Unguja na Dar, na waathirika wa kimbunga katika eneo la Kisiwapanza
kisiwani Pemba.
Taarifa ya Zancana imemalizia kwa kusema kuwa,
bado michango inaendelea kupokelewa, na kuwaomba wale wote wenye moyo na uwezo
kuchangia kwa kupitia accounti inayopatikana katika tovuti yao ya www.zancana.org

No comments :
Post a Comment