Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, May 11, 2015

Mahojiano na Mhe Alhaj Ali Hassan Mwinyi kuhusu KISWAHILI

   

Kiswahili inaaminika kuwa lugha asili ya Afrika inayozungumzwa na watu wengi zaidi kusini mwa jangwa la Sahara.
Nilugha ya taifa kwa nchi za Kenya na Tanzania na pia yazungumzwa kwenye nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Burundi, Rwanda, Uganda, Visiwa vya Comoro na nchi nyingine
Ikizungumzwa na watu wanaokadiriwa kufikia milioni 100 hivi sasa, Kiswahili ndio lugha pekee ya kiAfrika iliyo miongoni mwa lugha rasmi za Umoja wa Afrika.
Matumizi yake kama lugha inayozungumzwa na wengi katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati unaifanya lugha hii kuwa muhimu zaidi kwa watu wengi walio na mahusiano na / ama wanaotaka kujishughulisha na biashara, kazi ama diplomasia katika ukanda huo.
Kiswahili sasa kinafunzwa katika vyuo visivyopungua 50 hapa nchini Marekani, lakini pia inafundishwa kwenye vyuo vikuu mbalimbali Ulaya na hata bara Asia.
Ni lugha muhimu katika habari, shule, kazi za kiofisi, kidiplomasia na hata usalama miongoni mwa mataifa. Lakini , licha ya ukubwa wake, lugha hii inakabiliwa na changamoto mbalimbali.
Hivi karibuni, Chama cha Ukuzaji Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) kilifanya mkutano wake wa nne, ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Ali Hassan Mwinyi. Na amekuwa mkarimu sana kujiunga nasi kuzungumzia juu ya lugha yaKiswahili na changamoto zake.

No comments :

Post a Comment