dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, May 27, 2015

Mapya yaibuka sakata la Escrow.

Mbunge wa Ole (CUF), Rajab Mbarouk Mohamed.
Kashfa ya Escrow imeibuliwa upya bungeni baada ya wabunge kudai kuna kampuni ya Simba Trust inayomiliki asilimia 50 za kampuni ya Pan Africa Power (PAP), ambayo inadaiwa kuhusika katika ufisadi wa uchotwaji wa zaidi ya Sh.bilioni 300 katika akaunti ya Tegeta Escrow.
 
Hayo yaliibuliwa jana bungeni na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni wakati wa kuwasilisha hotuba yake ya kambi hiyo kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya mwaka 2015/2016 ya Wizara ya Viwanda na Biashara.
 
Msemaji wa kambi hiyo, Mbunge wa Ole (CUF), Rajab Mbarouk Mohamed, alisema wakati umma wa Watanzania unataka kuelewa wamiliki wa kampuni ya Simba Trust lakini katika hali ya kushangaza Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela), umegoma kutoa majina ya  wamiliki wa kampuni hiyo.
 
“Kambi rasmi ya upinzani tunaitaka serikali ieleze kwanini taasisi hii ya Brela iliyo chini ya wizara hii bado inakataa kutoa majina ya wamiliki wa Simba Trust, imekuwa kama ilivyokuwa makampuni yaliyohusika na uchotaji mabilioni ya Epa na fedha za mradi wa Meremeta,” alisema.Mnyaa alisema hatua ya Brela kukataa kutoa majina ya wamiliki wa kampuni hiyo kuna unganisha na dhana kwamba wamiliki wa kampuni hiyo ni viongozi wandamizi wa serikali ya CCM.
 
Alisema matatizo ya kiutawala yaliyopo katika sekta ya umma nchini yamesababisha sekta ya viwanda kushindwa kujiendesha kiushindani.
 
Aliongeza kuwa Shirika la Umoja wa Mataifa la na Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco), limebainisha kuwa viwanda vingi vinaendeshwa kwa hasara kutokana na kuwapo kwa gharama kubwa za uzalishaji, tija ndogo, riba kubwa za kibenki,tatizo la umeme na urasimu. 
 
Mnyaa alisema licha ya kwamba Shirika la Viwango Tanzania (TBS), lipo lakini takwimu zinaonyesha kuwa Tanzania inaongoza kwa kuwa na bidhaa feki kwa ukanda mzima wa kusini na mashariki mwa Bara la Afrika.
 
“Tukio la hivi karibuni kampuni ya UNI-METAL EAST AFRICA Co iliingiza bandarini mabati feki 100,000 na TBS ikakamata mabati feki 15,000 tu na 75,000 yaliyobaki yalikuwa tayari yameingia kwenye mzunguko na Watanzania walikuwa wameshanunua mabati hayo,” alisema.
 
Awali Dk. Kigoda alisema serikali imeandaa utaratibu ambao utawezesha kuwapatia wafanyabishara wadogo maarufu wamachinga leseni maalum ili watambuliwe na kuondokana na adha ya kunyanyaswa katika maeneo wanayofanyia biashara zao.
 
Dk. Kigoda alisema moja ya mikakati ya wizara katika kipindi cha 2015/2016 ni pamoja na kufufua viwanda vilivyobinafsishwa ambavyo havifanyi kazi kikamilifu kikiwamo kiwanda cha matairi cha General Tyre cha jijini Arusha na kiwanda cha nguo Urafiki. 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment