dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, May 16, 2015

Matayarisho ya Mapokezi ya Rais wa Msumbuji Zanzibar Yakamilika.

  1. Image result for Filipe Jacinto Nyusi of mozambique
  2. Filipe Nyusi
    President of Mozambique
  3. Filipe Jacinto Nyusi, also spelt Nyussi, is the fourth President of Mozambique, in office since 2015. He previously served as Minister of Defence from 2008 to 2014. 
  4. Born: February 9, 1959 (age 56), Mueda District, Mozambique
  5. Office: President of Mozambique since 2015
  6. Spouse: Isaura Nyusi
  7. Party: FRELIMO
  8. Presidential term: January 15, 2015 –
  9. Education: Victoria University of Manchester, Brno University of Technology, University of Manchester

Na Othman Khamis OMPR.

Matayarisho kwa ajili ya ujio wa Rais wa Jamuhuri ya Msumbiji Bwana Philipe Jacinto Nyusi anayefanya ziara rasmi ya Kiserikali Nchini Tanzania yamekamilika kwa  upande wa hapa Zanzibar.

Bw. Nyusi anaiongoza  Jamuhuri ya Msumbiji katika kipindi cha Miaka Mitano baada ya kuingia Madarakani  kwenye Uchaguzi Mkuu wa Nchi hiyo wa Tarehe 15 Oktoba mwaka 2014 Kupitia chama Tawala cha Frelimo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya  Sherehe na Maadhimisho  ya Kitaifa alipata fursa ya kukagua matayarisho hayo yaliyoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania { JWTZ } pamoja na vikundi vya burdani.

Matayarisho ya mapokezi hayo yamefanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amaan Karume ambapo Nyimbo za Taifa za Msumbiji na   wa Zanzibar ziliiimbwa zikiambatana na mizinga 21 ya majaribio kupigwa kuashiria kukamilika kwa maandalizi hayo.

Bwana Philipe Nyusi anayetarajiwa kupokelewa rasmi na mwenyeji wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Braza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein mchana wa Jumatatu ya Tarehe 18 Mei mwaka huu atapata fursa ya kupokea saluti na kukagua gwaride rasmi lililotayarishwa kwa heshima yake.Katika mapokezi hayo Dr. Shein anatarajiwa pia kuambatana na Viongozi mbali mbali wa Serikali, Kisiasa, wananchi pamoja na Raia wa Msumbiji wanaoishi hapa Zanzibar .
Bwana Philipe Jacinto Nyusi aliyezaliwa  Tarehe 9 Febuari mwaka 1959  katika Kijiji cha Namai kwenye Jimbo la Cabo Delgado ndani ya Wilaya ya Mueda Nchini Msumbiji akitokea katika familia ya wazazi waliopigania uhuru wa Taifa hilo kutoka kwa Wareno ana stashahada ya Uhandisi ya chuo Kikuu cha Manchester Nchini Uingereza .

Kiongozi huyo wa Msumbiji Bwana Nyusi kabla ya kuwa Waziri wa Ulinzi wa Msumbiji kuanzia Tarehe 27 Machi mwaka 2008 hadi 2014 aliwahi pia kuwa Mhadhiri katika Kampus ya  Nampula ya chuo Kikuu cha Pedagogica.

Kiongozi huyo wa Jamuhuri ya Msumbiji Bwana Philipe  Jacinto Nyusi anakamata wadhifa huo akiwa Rais wa Nne Tokea Taifa hilo kutoka mikononi mwa Ureno akitanguliwa na Kiongozi wa kwanza wa Ukombozi Rais  Samora Machel, Bw. Joaquim Chisano pamoja na Bwana Armando Guebuza.

Bwana Nyusi  mwenye umri wa miaka 56  akiwa ni Rais wa 4 kuchaguliwa Kidemokrasi Nchini Msumbiji wazazi wake walimvusha kupitia Mto Ruvuma na kuingia Nchini Tanzania kupata elimu yake ya awali katika  Skuli ya Msingi ya Frelimo Tunduru Nchini Tanzania.

Alifanikiwa kuendelea na masomo yake ya Sekondari kwa kujiunga na Skuli ya Frelimo ya Mariri iliyopo Cabo Delgado na baadaye Sekondari ya Samora Mashel Mjini Beira.

Mwaka 1973 Bwana Philipe Nyusi aijiunga na Chama cha Frelimo akiwa na umri wa Miaka 14 na kujiingiza katika masuala ya kisiasa na baadaye kupata mafunzo ya kijeshi  katika Kambi ya mafunzo ya Nachingwea Nchini Tanzania.

Akiwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya Ukombozi wa Frelimo Bwana Philipe Nyusi alipata mafunzo ya Uongozi katika Mataifa ya India, Afrika Kusini, Swaziland na Marekani.

Mwaka 1990 Bwana Philipe Nyusi alikamilisha mafunzo yake  ya Shahada ya kwanza ya Uhandisi  katika chuo kikuu cha Ufundi cha Brno iliyokuwa Czechoslovakia. Pia alipara stashahada ya Uongozi katika Chuo Kikuu cha  Manchester Nchini Uingereza.
Kwenye Utumishi wa Umma Bwana Nyusi aliwahi kufanya kazi katika Mamlaka ya 

Bandari na Reli ambapo utendaji wake ulimuwezesha kuchaguliwa kuwa Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka hiyo baadaye kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa Bodi ya Mamlaka hiyo.

Mnamo Tarehe 1 Machi 2014 Kamati Kuu ya Taifa ya Chama cha Frelimo ilimchaguwa Bwana Philipe Nyusi kuwa mgombea wa chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa Nchi hiyo baada ya kupata asilimia 68% ya kura dhidi ya mgombea mwenzake wa chama hicho Bibi Luisa Diogo aliyepata asilimia 31%.

Hiyo ilikuwa raundi ya pili ya kumtafuta Kinara wa Frelimo atakayeipeperusha Bendera ya Chama hicho kwenye   uchaguzi Mkuu wa Vyama vingi Nchini Msumbiji wa 2014 baada ya ile ya kwanza  aliyopata asilimia 46% chini ya kiwango kinachokubalika kwa mujibu wa Katiba ya Nchi hiyo cha asilimia 50%.

Bwana Philipe  Jacinto Nyusi alifanikiwa kueperusha Bendera ya Chama cha Frelimo baada ya kushinda Uchaguzi Mkuu wa Tarehe 15 Oktoba mwaka  2014 kwa kupata Kura Milioni 2,778,497 sawa na asilimia 57.03%.

Aliwashinda Wapinzani wake Bwana Afonso Dhlakama wa Chama che Renamo aliyepata kura Milioni 1,783,382  sawa na asilimia 36.61% akishika msindi wa  Pili na Bwana Dayiz Simango wa Chama cha MDM aliyepata Kura Laki 309,925 sawa na asilimia 6.36%.

Kiongozi huyo wa Jamuhuri ya Msumbiji Bwana Philipe  Jacinto Nyusi anakamata wadhifa huo akiwa Rais wa Nne Tokea Taifa hilo kutoka mikononi mwa Ureno akitanguliwa na Kiongozi wa kwanza wa Ukombozi Rais  Samora Machel, Bw. Joaquim Chisano pamoja na Bwana Armando Guebuza.

No comments :

Post a Comment