
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, amesema licha ya muda wa vikao vya Bunge kubadilika na kutumia saa nyingi zaidi kuliko ilivyokuwa hapo awali, wabunge hawatalipwa posho ya ziada.
Alitoa ufafanuzi huo kufuatia baadhi ya watu kuliuliza iwapo muda wa bunge hilo unaoanza saa 3:00 asubuhi hadi saa 8:00 mchana , kisha kurudi tena saa 10 hadi saa 2:00 usiku kuna nyongeza ya posho?
“Mabadiliko ya ratiba hayana uhusiano na mabadiliko ya posho. Wabunge hawalipwi malipo ya ziada ‘over time’ wala hawalipwi kwa saa”.
Aliongeza kuwa posho za kujikimu na vikao zimebakia kama zilivyokuwa hapo awali ambako, walikuwa wanaanza kikao saa 3:00 asubuhi hadi saa 7:00 mchana na kurejea tena saa 11 jioni hadi saa 1:45 usiku.
Wabunge wanaelezwa kusaini Sh. 150,000 kila siku ikiwa ni posho ya kujikimu ya Sh. 80,000 na 70,000 kwa ajili ya vikao.
Kiasi hicho ni tofauti na posho za madereva, mafuta pamoja na gharama nyingine ambazo wanalipiwa na serikali.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment