dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, May 5, 2015

PELEKA PESA ZA RAMADHANI NYUMBANI WIKI HII, KWANI EXCHANGE RATE NI NZURI SANA!

Hizi ni exchange rates zilizopita. Rate ya leo ni nzuri zaidi. 
1CAD$ = 1600/- kupitia online services za PBZ Ltd.

Benki Kuu (BoT) ya Tanzania imeuza Dollar kama milioni 339 kutokea January mpaka April, mwaka huu, lakini mwaka huu wafanya biashara wameagizia mali nyingi sana kutoka nje na kwahivyo Dollar zinatakiwa sana na zinanunuliwa kwa bei ya juu kutokana na uhaba.

Kama unataka kuwakumbuka wazee na jamaa nyumbani hasa kwaajili ya Ramadhani tunayoitegemea tarahe 19 Juni, basi sasa ndio wakati mzuri wa kutuma pesa nyumbani.

Dollar moja ya Canada kwa leo utapata kama TShs 1,600/- na Dollar ya Marekani inazidi TShs 2,050/-.

Exchange rate hii nzuri ya kupeleka pesa nyumbani haitobakia hivi hivi siku zote. Kesho Benki Kuu (BoT) wakianza kuuza Dollar basi tutarejea pale pale kwenye rate ya TSh 1450/- kwa Canadian Dollar moja.

Kwahivyo, bora kila mtu awahi wiki hii kupeleka pesa za kuwasaidia wazee, ndugu na jamaa zetu nyumbani kwa futari kabla exchange rate haijageuka!

1 comment :

  1. Zanzibar Ni Kwetu, ahsanteni kwa kutujulisha. Tayari tunaona zishaanza kupungua!

    ReplyDelete