Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, May 16, 2015

Sumaye 'atabiri' machafuko Uchaguzi Mkuu 2015.

Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye.
Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, ameonya kuwa taifa linakabiliwa na hatari ya machafuko ikiwa hakutakuwa na udhibiti wa rushwa na ufisadi vinavyochochea ubinafsi badala ya kukidhi matakwa yenye maslahi kwa umma.
 
Sumaye aliyasema hayo kwenye hotuba yake aliyoitoa wakati akizungumza katika mkutano ulioratibiwa na serikali ya wanafunzi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii (ISWOSO) jijini Dar es Salaam jana.
 
Kwa mujibu wa Sumaye, hali kama hiyo isipopigwa vita na kudhibitiwa itapanda mbegu ya chuki na mapambano kati ya wenye nacho na wasio nacho, wanaoongoza na wanaoongozwa ama wenyeji na wageni.
 
“Ili mradi kundi moja linahisi matatizo yake yametokana na hilo kundi  lingine hata kama siyo kweli. Dawa ya uhakika ya matatizo haya ni kuwa wazalendo wa kweli kwa nchi yetu na kuwa watumishi wema wa umma walioweka umma mbele na nafsi zetu baadaye,” alisema.
 
UCHAGUZI MKUU 2015
Alisema ikiwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu hautafanyika kwa haki na uwazi, unaweza ukasababisha machafuko kama ilivyo kwa nchi nyingine hususani za barani Afrika.Alisema vijana wana wajibu mkubwa katika uchaguzi huo na kuonya kuwa hivi sasa fedha zinatembezwa kila kona ya nchi ili kusaka kura.
 
Kwa mujibu wa Sumaye, matumizi ya fedha yameshaelezwa kutokea kwa wajumbe wa vikao vinavyopitisha majina ya wanaotaka kuwania uongozi  ikiwamo Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa.
 
“Rushwa hii ya kusaka madaraka ya kisiasa ina athari kubwa kwa umma na nchi kwa ujumla. Mara nyingi anayefanya hivyo ana uchu na uroho wa madaraka kiasi kwamba yuko tayari kufanya lolote na chochote ili apate hayo madaraka anayoyahitaji,” alisema.
 
Alisema ikiwa utaratibu wa kununua uongozi utaachwa utumike, mhusika akishinda anakosa mamlaka ya kimaadili kuwahudumia waliompigia kura kwa sababu kilichofanyika ni biashara.
 
Alisema, “kama amezipata kwa rushwa akishapata madaraka atakula rushwa kubwa zaidi ili fedha zake zirudi na faida kubwa. Hakuna mtoa rushwa asiye mla rushwa. Kama fedha hizo zimetokana na matajiri, basi kipaumbele cha kuwahudumia watakuwa waliomuwezesha na atalipa fadhila mpaka fedha zao zirudi na faida kubwa.”

CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment