Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, June 19, 2015

Aina za kampuni unazoweza kumiliki

Kambole 
Aina kutokana na umiliki. Kwenye aina hii kuna aina mbili ambazo ni kampuni binafsi na kampuni ya umma.
Ndugu msomaji wa Uwanja wa Kambole, leo tutajikita kwenye aina za kampuni zinazotambuliwa na sheria namba 12 ya mwaka 2002. Kuna aina mbalimbali za kampuni na zinatofautiana kulingana na uhitaji na malengo ya mtu anayefungua pia akipata ushauri wa mwanasheria wake. Zifuatazo ni aina za kampuni Tanzania.
Aina kutokana na umiliki. Kwenye aina hii kuna aina mbili ambazo ni kampuni binafsi na kampuni ya umma.
Kampuni binafsi (private company) ni ile ambayo kwenye katiba yake yametamka wazi kuwa yatakuwa ni kampuni binafsi na sifa zake ni pamoja na hayawezi kuuza hisa kwa umma, lakini pia haki ya kuuza hisa haipo huru pia idadi ya wanahisa haitakiwi kuzidi watu hamsini kwa mujibu wa kifungu cha 27 cha Sheria ya kampuni namba 12 ya mwaka 2002.
Kampuni ya umma (public company) ni kampuni ambayo katika katiba yake imeelezwa kuwa haya yatakuwa ni kampuni ya umma, hii ina maana kuwa wanahisa wake hawana ukomo kwa idadi, lakini pia haya kuuza hisa kwake kuko huru na kwa yeyote muda wowote. Kampuni hizo ni zile zinazoruhusu kuuza hisa zao kwenye soko la hisa la Dar es Salaam, lakini hii haina maana kuwa haya ni kampuni ya serikali.
Aina kutokana na utaifa. Kampuni ya kigeni (foreign company), kwa upande wa sheria za kampuni zimesajiliwa nje ya nchi na yanafanya kazi Tanzania. Sheria imeweka wazi kuwa hii itakuwa ni kampuni ya kigeni na yana utaratibu wake wa usajili, utaratibu huo umeelezwa chini ya kifungu cha 433 mpaka 449 cha sheria ya kampuni ya mwaka 2002, nitaeleza vizuri kwenye mada zijazo. Lakini kwa mujibu wa sheria ya ardhi ya mwaka 1999, kampuni ya kigeni ni ile ambayo hisa zake nyingi zinamilikiwa na wageni kuanzania asilimia 51.
Kampuni ya wazawa (local company) hizi ni kampuni ambazo zimesajiliwa ndani ya nchi kwa lengo la kufanya shughuli zake ndani ya nchi na ina haki nyingi zaidi ya kampuni ya kigeni kwa mfano haki ya kumiliki ardhi.
Aina kutokana ukomo wa madai
Kampuni yenye ukomo (limited company) hapa tuna ina mbili za ukomo, ukomo wa hisa na ukomo wa dhamana.
Kampuni yenye ukomo wa hisa (Limited by shares) ni yale kampuni ambayo katiba yake imeeleza kuwa yatakuwa na ukomo wa madai kwa hisa, haya kampuni wanahisa wake watalazimika kuchangia hisa ili kampuni iendelee na kuzilipia, endapo kampuni itakuwa imeelemewa na madeni watatakiwa kuchangia kiasi kile cha fedha ambacho hawajakilipia kwenye hisa zao kwa mujibu wa idadi ya hisa walizochukua.
Kampuni yenye ukomo kwa dhamana (Limited by guarantee) haya ni kampuni ambayo yanaendeshwa na kusajiliwa kama taasisi zisizokuwa za serikali (NGO) na kampuni inakuwa na haina hisa ila ni dhamana tu kwa wamiliki wake, pale wamiliki wake watatakiwa kuchangia kile kiasi walichoweka kama dhamana ni kampuni inapoelemewa na madeni. Aina hii ya kampuni inakuwa haina hisa ila inategemea misaada na ufadhili kutoka kwa watu mbalimbali.
Kampuni isiyo na ukomo (unlimited company) Hii ni aina ya kampuni ambayo wanahisa wake hawana ukomo wa madai endapo kampuni itakuwa imekumbwa na madeni, sijawahi kuiona kampuni hii na kama zipo basi zipo chache, wengi hupendelea kampuni ambazo zina ukomo kutokana na mahitaji yake.
Mwandishi wa Makala hii ni Jebra Kambole Wakili wa Kujitegemea kutoka Kampuni ya uwakili ya Law Guards Advocates
/Mananchi.

No comments :

Post a Comment