Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, June 7, 2015

Mama asoma shule ya msingi na wanaye watatu

Aisha akiwa na watoto wake shuleni baada ya muda wa masomo.Kushoto ni Godgift Shani (5), katikati Philomena Shani (9) Tecla Shani (3) . 
Aisha ni mama na mwanafunzi wa Shule ya Msingi Meru iliyoko Arusha, ni mwanafunzi wa darasa la tano akiwa anasoma na watoto wake watatu katika shule hiyo.
Wanafunzi waliotakiwa kujiunga darasa la kwanza mwanzoni ilikuwa ni wale waliofikisha umri si chini ya saba hadi 13, ikiwa ni pamoja na kuangaliwa kama mkono wa kulia unaweza kushika sikio.
Baada ya kuboreshwa kwa sera na mikakati ya elimu Serikali iliweza kuanzisha elimu ya watu wazima ambao uliitwa Mpango wa Elimu ya Msingi kwa Waliokosa Elimu (MEMKWA), ambao umetoa fursa kwa kila mwananchi kupata haki yake kikatiba ya kupata elimu.
Mpango huo umeweza kusaidia wengi akiwemo Aisha Shani (25) ambaye amejikuta akisoma shule moja na watoto wake watatu, jambo ambalo watu wengine wanaona ni gumu na hawaamini kama ameamua kutimiza haki yake ya kikatiba ya kupata elimu kupitia mpango huo.
Japo wengi walimuona kuwa ni chizi na hata familia ya upande wa mume wake, kuona kuwa maisha yamewashinda na watu kumshauri apelekwe akasome masomo ya ufundi, familia ya Shani Malepu haikukubali hilo.
Mjue Aisha
Aisha ni mama na mwanafunzi wa Shule ya Msingi Meru iliyoko Arusha, ni mwanafunzi wa darasa la tano akiwa anasoma na watoto wake watatu katika shule hiyo.
Mtoto wake wa kwanza Pholomena Shani (9) yuko darasa la nne, Godgift Shani darasa la kwanza na Tecla Shani chekechea shuleni hapo.
Akizungumzia historia ya maisha yake alisema yeye ni mtoto pekee katika familia yake ambaye alishi maisha magumu baada ya kuondokewa na mama yake akiwa na miezi miwili. Kulingana na ugumu wa maisha alijikuta anaishia kulelewa na dada yake wa kwanza ambaye baba yake mzazi mzee Ally alimuamuru aache shule ili amlee mdogo wake(Aisha).
Baada ya kufikisha miaka sita na dada yake aitwaye Siwema kuwa na miaka 13 walipelekwa kuanza shule, lakini dada yake alikataliwa kwa madai alikuwa na umri wa miaka 16.
Baada ya hapo baba yao alikata tamaa ya kuwasomesha na kujikuta wameishia kukaa nyumbani.
Kutokana na changamoto za maisha kwenye familia, Aisha alijikuta anakuwa mfanyakazi wa ndani kwa miaka miwili akiwa na umri wa miaka 15.
Aisha anasema hakupenda kazi za ndani kwasababu alikuwa bado mdogo, hivyo alipelekwa kulelewa na shangazi yake mkoani Morogoro.
Hata hivyo Aisha anasema shangazi yake huyo alifariki dunia na kujikuta anarudi tena kuwa mfanyakazi wa ndani na mwaka 2007 alipata ujauzito na kuamua kuolewa.
Akizungumza sababu ya yeye kurudi kusoma anasema alipenda kusoma, lakini mwanzoni hakupata fursa hiyo akiwa kwa baba yake kutokana na ugumu wa maisha, hivyo kuwa kwa mume wake kumemfanya atulie na kuwaza kurudi shuleni.
“Nilikuwa na uchungu sana wa kupata elimu, nilikuwa nawaangalia wenzangu wakienda shule natamani sana, sema maisha yangu yalikuwa ni ya kuhamahama na kufanya kazi za ndani,”anasema Aisha.
“Nilipomwambia mume wangu nataka kusoma, hakunipinga na yote ni kwasababu mume wangu anapenda kusoma, japo mtaani waliniita chizi na wengine kusema vibaya sikukata tamaa.”
Anasema alianza shule mwaka 2014 kutokana na kujua kusoma na kuandika alianzia darasa la nne na si la kwanza, japo ilikuwa ngumu kwa walimu kuamini kama ningeweza kusoma shule ya msingi lakini nimeweza sana.
Mume wake Aisha aitwaye Shani akizungumzia mkewe kusoma anasema mke wake ni mpenda maendeleo na kujua kusoma na kuandika alijifunzia kutoka kwa mtoto wake wa kwanza Philemona ambaye alikuwa anamfundisha mama yake kusoma.
“Mke wangu amejua kusoma kupitia kwa mtoto wake, alikuwa anapenda sana kujua anafanyaje kazi zake za shule kila jioni alikuwa anamsii wakasome, baada ya kusema anataka kusoma sikumzuia kwakuwa nilijua anachokipenda,”alisema Shani.
“Mke wangu atakuja kuwa mwalimu, nitamsaidia asome hadi atakapochoka kwakuwa nimeona ndoto yake ni kuwa mwalimu na nitahakikisha ndoto yake imekamilika kwa ajili ya maendeleo ya familia yetu.”
Uamuzi wa Aisha kusoma umeleta changamoto nyumbani kwake kwa kuwa imebidi waishi nyumba tofauti kutokana na umbali wa shule yenyewe.
Aisha anasema kutokana na umbali wa eneo analoishi na gharama wamemuacha mume wake nyumba waliojenga, na yeye pamoja na watoto wake wanakaa kwenye duka wanalouza bidhaa ili iwe karibu na barabarani ambako ni rahisi kwa wao kufika shuleni.
“Kuamua kukaa karibu na barabarani ni kuepusha gharama ambako mimi pamoja wanangu kwa siku tunatumia zaidi ya Sh 1,200 ya nauli, kama nitakuwa nakaa kwangu itanibidi niwe napanda bodaboda,”anasema.
Pamoja na viboko kuwa ni nembo ya shule kwa wanafunzi watukutu, Aisha naye anakabiliwa na hilo ambapo anasema haoni aibu kuchapwa kama amekosea na pia huwa anachapwa mara nyingi na watoto wake wanamshuhudia akichapwa. “Watoto wangu huwa wananiuliza kila siku kwanini nikichapwa huwa silii, huwa nawaambia kwasababu mimi mkubwa na wengi hasa mwanangu wa chekechea akiona nachapwa huwa ananikimbilia kunipa pole.”
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Meru, Musa Luambano anasema anafarijika kuona wananchi wana hamasa ya kupata elimu na yeye amekuwa mstari wa mbele kumsaidia Aisha.
“Michango midogomidogo kama ya mitihani, masomo ya jioni na mingineyo tumemuondolea yeye pamoja na watoto wake, yeye analipa ada tu, tumeamua kufanya hivyo ili kuhakikisha anafikia lengo lake,”anasema.
“Aisha ni mwanafunzi aliyekuwa na umri mkubwa hapa shuleni kwangu, ila ninao wengine kama ishirini pia lakini wote wanatoka katika maisha magumu na hasa wengi ni wale ambao walikuwa wanafanyishwa kazi za ndani, ama kuzalishwa ila Aisha ni peke ambaye ameolewa na anamaisha yake.”
Shule ya Meru ni shule ambayo pia ni kituo kinachotoa masaada kwa wanafunzi hasa wale wanaoishi katika mazingira magumu, ombaomba na wale wanaosoma elimu maalum bubu na viziwi.

No comments :

Post a Comment