AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, July 4, 2015

Dk. Kalokola: Msafara wa JK umekwamisha ndoto yangu

Dk. Muzzamil Kalokola
Siku moja baada ya CCM, kufunga zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kuomba kuteuliwa  kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa Oktoba, mtangaza nia Dk. Muzzamil Kalokola, amerejesha fomu kwa kuchelewa akidai amekwamishwa na msafara wa Rais Jakaya Kikwete.
Dk. Kalokola alirejesha fomu hiyo jana mchana mjini Dodoma . Mtangaza nia huyo na wenzake, Mwalimu Anthony Chalamila, Helena Elinewinga na Peter Nyalali mtoto wa Jaji Mkuu mstaafu wa Tanzania, hayati Francis Nyalali, walishindwa kurudisha fomu hizo juzi jioni ambao ulikuwa muda wa mwisho.
Mtangaza nia akiwa anatumia gari binafsi, aliwasili jana makao makuu ya CCM mjini Dodoma, saa 1:30 asubuhi, akimtafuta Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bara, Rajab Luhwavi; lakini alikwama hadi saa 7:25 mchana alipokabidhi fomu hiyo kwa mmoja wa maofisa wa Ofisi ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) na Oganaizesheni.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara,Rajab Luhwavi, alitangaza kuchora mstari mwekundu wa kutoendelea kupokea fomu hizo, juzi saa 10:00  jioni; baada ya Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba kurejesha fomu yake.
Alipotafutwa na NIPASHE kwa njia ya simu ili kueleza kilichomsababisha achelewe kurejesha fomu hiyo hadi zoezi hilo linafungwa rasmi Julai 2, mwaka huu, Dk. Kalokola alisema:
“Nimewaeleza ukweli kwamba nilikwama Morogoro kwa saa zaidi ya nne nikisubiri msafara wa Rais Jakaya Kikwete upite, ndiyo tukaruhusiwa kuondoa magari yetu, ningewezaje kuwahi deadline. Nashukuru Mungu wamenielewa baada ya kubishana kwa muda mrefu. Hivi ninavyoongea na wewe niko njiani naelekea Dar es Salaam,” alisema.
Alieleza kuwa:Hata huyo niliyemkabidhi fomu yangu simjui jina, isipokuwa ni Ofisa wa Idara ya NEC na Oganaizesheni Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Kuna vitu vinashangaza lakini ilinibidi niwaombe wasininyime haki yangu ya kurejesha fomu kwa kuwa niliichukua nikiomba kuteuliwa kugombea.”
Hata hivyo, Naibu Katibu Mkuu Luhwavi, alipotafutwa ili kutoa ufafanuzi hakupatikana.
CHALAMILA
Alipoulizwa sababu za kushindwa kurejesha fomu hizo, alisema ameshindwa kufanya hivyo kutokana na ubaguzi uliopo ndani ya CCM. Chalamila Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa Wilaya ya Morogoro Mjini (NEC) alichukua fomu hiyo Juni 27 zikiwa zimebakia siku sita za kusitisha zoezi hilo.
Akizungumza kwa njia ya simu, Chalamila alisema ubaguzi huo unatokana na viongozi wa CCM kuruhusu mtangaza nia kudhaminiwa na wadhamini zaidi ya 450  ambao wametajwa kinanuni; hali ambayo imemsabaishia yeye kila anapofika mikoani kukosa wadhamini, akiambiwa hakuna wa kumdhamini, kwa kuwa tayari wameshamdhani mgombea mwingine.
"Hata kama muda umeisha lazima nirudishe fomu hizo ili kuweka historia na kumwambia Katibu Mkuu wa CCM (Abdurahman Kinana), kwamba ndani ya chama kuna makundi na kuna tatizo la kuangaliana kwa upendeleo; kwamba huyu ni bora na huyu hafai, hali hii itakiua chama," alisisitiza Chalamila.
Kwa upande wake, Hellena Dinah Elinewinga ambaye naye alipoteza sifa za kuomba kuteuliwa na CCM, kugombea kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu; aliiambia NIPASHE kwa njia ya simu kuwa,
”Niliacha kurejesha fomu yangu, kwa sababu nilishindwa kutafuta wadhamini kwa vile, wahusika wakuu wa chama changu, hawakuona umuhimu wa kunipatia mafunzo kabla ya kwenda kusaka hao wadhamini. Nilitaka wanipe mafunzo pia juu ya upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kampeni; …unajua kulikuwa na tetesi, eti huwezi kudhaminiwa kama huna pesa,” alihoji Elinewinga.
Hadi CCM inafunga zoezi hilo, wagombea waliokuwa wamefanikiwa kutimiza masharti ya kuchukua na kurejesha fomu hizo ni 38 pekee.
Mfululizo wa vikao vya juu vya maamuzi vya CCM vitatanguliwa na Kikao cha Sekretarieti ya Kamati Kuu ambacho kitafanyika Julai 7, mwaka huu, kikifuatiwa na Kamati ya Usalama na Maadili, Julai 8; huku Kamati Kuu (CC) ikikutana Juali 9 na kufuatiwa na Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Julai 10 na baadae kuhitimishwa na Mkutano Mkuu wa Taifa wa chama hicho utakaofanyika Julai 11 na 12 mwaka huu. 
CHANZO: NIPASHE


No comments :

Post a Comment