dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, July 28, 2015

Lowassa ajiunga rasmi na Ukawa, akabidhiwa kadi ya uanachama Chadema

Edward Lowassa (Kushoto) akiteta jambo na Profesa ibrahim Lipumba (Kulia) katika Mkutano uliofanyika katika hoteli ya Bahari Beach Jijini Dar es Salaam

Aliyekuwa waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa ametangaza rasmi kuhama CCM na kujiunga na Ukawa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema.


Lowassa ametangaza uamuzi huo leo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar na kusema amekubali mwaliko wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Amesema kuwa CCM haikumtendea haki katika kupitisha majina ya wagombea urais hivyo hawezi kuendelea kubaki kwenye chama hicho ‘’ Niliwekewa mizengwe kuhakikisha Jina langu halifiki Kamati Kuu na Halmashauri Kuu’’.

Waziri Mkuu huyo wa zamani ameeleza kuwa nia yake ni kuleta mabadiliko hivyo kujiunga na Chadema ni kuendeleza nia yake ya kuwatumikia Watanzania ‘’ CCM Si baba yangu wala Mama yangu, Watanzania kama wameyakosa mabadiliko ndani ya CCM, basi watayapata nje ya CCM’’

Aidha ameongeza kuwa hajakurupuka kufanya uamuzi huo na kuendelea kubaki ndani ya CCM itakuwa ni unafiki ‘’ Sijakurupuka kwa uamuzi huu hivyo basi kuanzia leo natangaza rasmi kuondoka CCM na kujiunga na UKAWA kupitia Chadema’’ alisema Lowassa.

Hata hivyo muda mfupi baada ya kutangaza uamuzi huo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alimkabidhi Lowassa kadi ya uwanachama.
/Mwananchi.

No comments :

Post a Comment