dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, July 28, 2015

Press conference: Lowassa atambulishwa kwa ukawa-maswali na majibu!



Written by jazba
Baada
ya kuwashukuru viongozi wa ukawa kwa kumpokea na familia yake na viongozi wa kidini,watu na wnachama wote wanaomuunga mkono anaendelea na kusema;

“uchaguzi wa CCM ulifanywa kwa upendeleo na chuki iliokithiri dhidi yangu. Viongozi walikuwa tayari kupanda mbegu ya chuki na mifarakano, yaliyotokua Dodoma yameitia dosara nchi yetu. Nimenyimwa haki ya unapotuhumiwa unajitetea, natural justice.
CCM niliyoiona Dodoma sio chama kile nilichokuliwa na kilichojengwa katika misingi, nasema sasa basi, Nyerere alisema CCM sio baba yangu na wala si mama yangu na alisema mkikosa mabadiliko nje ya CCM hivyo basi baada ya kutafakari kwa kina nimeamua naondoka CCM na kuitikia wito wa UKAWA na kujiunga na chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA. 

Na nawashukuru viongozi wa vyama vya upinzani kuona kuwa naweza kutoa mchango wangu.
Natoa wito kwa watanzania wenye nia njema, kujiunga nasi kuleta maendeleo ya taifa, Safari ya matumaini inaendelea kuwepo kwa kupitia UKAWA, lakini safari hii haiwezi kukamilika bila kujiandikisha hivyo twende kujiandikisha. Nimesikia tetesi wanakaribia kufunga, naomba tume ya uchaguzi waongeze muda kama walivyoongeza Njombe ili wakazi wote wa Dar waweze kujiandikisha.

MASWALI NA MAJIBU

mwandishi: Lowassa unahama kwenda kulipiza visasi endapo utashindi lakini pia wapo wanasema una ukaribu na matajiri wengi katika nchi hii, He, Ukishinda hutaamisha rasimali kwa matajiri

Lowassa: Nachukia sana umasikini, natamani watanzania wawe matajiri, wawe kama kina Mengi na mzee wa Azam. Marekani kuna matajiri wengi, unawataka wawatupe chooni.Umefanya nini mpaka uogope kulipiwa kisasi, waulizeni wamefanya nini mpaka waogope mimi kulipa kisasi. Lakini mimi ni mkristo, samehe saba mara sabini hivyo kama wana madhambi yao wakamuombe tu Mungu wao.

mwandishi: Je, Ikiwa watanzania watawapeni ridhaa, tumeshuhudia bunge letu limepisha sheria mbovu na mikataba, mtabadilisha hilo?

Lowassa: Naona hili panoge tushirikiane sote, namp
Tutumie rasilimali kwa wananchi wote, mikata na mikataba iliopitishwa itatazmwa upya ili wananchi wote tunufaike na rasilimali hizi

Makaidi: Tutaangalia sababu walizopitishia na tuone ni kwa nia njema au mbaya na ikiwa mbaya tutafumua sheria zote.

Mbowe: Kama tuna hasara moja kubwa tunaipata kama taifa, ni kuwa na bunge linalotoka kutoka chama kimoja, absolute majority. Kwa namna CCM kimekuwa na wabunge wengi, kimekuwa kinaangalia maslahi ya chama chao kuliko ilivyo kwa taifa. Bunge la kumi na moja litakuwa na uwiano wa kuridhisha hivyo watu watashindwa kufanya maamuzi kwa maslahi ya vyama vyao

Mbatia: Rasimu ya pili ya katiba yetu ambayo ndio imetufanya kuwepo UKAWA. Tunawahahakishia watanzania, tutaweka mfumo wa kikatiba kwamba serikali yoyote itayokuwa madarakani ifate maagizo ya Bunge. Nashukuru sana Lowassa kujiunga

mwandishi: Wakati wa Richmond ulikua na matatizo na hivi vyama, Je usipotimiza walivyotarajia?

Lowassa: Am sick of Richmond, mtu yoyote mwenye ushahidi wa mimi kuhusika Richmond aende mahakamani, kama huna just shut up. Nilichukua uamuzi kwa niaba ya serikali.

Nimeondoka madarakani miaka nane iliopita, mambo haya yameongezeka yamepungua, mikono yangu ni misafi na mtu mwenye ushahidi acha kupigapiga kelele, peleka mahakamani

Lowassa na familia yake wanakabidhiwa kadi

UKAWA WAMKARIBISHA LOWASSA

Makaidi:
Salamu zangu fupi tu, kwanza kwa bwana Mbowe nimpongeze kwa kuweza kutuletea kifaa, bwana Lowassa na nampongeza Lowassa baada ya kuona kiza mbele akaamua kuja kwetu, simfahamu sana mzee Lowassa lakini namfahamu kupitia kwa mwanangu amefanya kazi na Lowassa. Viongozi wa UKAWA tutakuwa pamoja nae kuhahakisha CCM mnaondoka, kwa pamoja tutaweza kuiondoa CCM tarehe 25 Oktoba. Nashukuru sana Lowassa kuamua, ukiona njia ina matatizo, unabadilisha. Kama amekuja kutukwamua, watu wote tutamsikiliza.

Juma Duni: Kazima niseme nimepigwa na butwaa, Lowassa karibu katika ukawa na tumepata fahari, na kwa lugha ya kisasa tumepata jembe na Oktoba patachimbika, CCM wamesahau kabisa hata malengo ya kugombea uhuru. Tuna wajibu pamoja wewe kurudi katika misingi ya kupigania uhuru nchi hii, na leo nimefurahi kusikia na wewe umasikini huupendi. Sote tuliokaa hapa ni watoto wa masikini, Lowassa tunapata fahari kubwa kuwa nawe, CUF tutashirikiana. Mkapa alisema Zanzibar hakuna mtu mwenye hatimiliki ya nchi hii, hamna kikundi chochote kina hatimiliki wa nchi hii.

Mbatia: Haki zako kama waziri mkuu ukihamia UKAWA haziondoki, UKAWA tutazilinda. Mpaka leo UKAWA tupo pamoja, watanzania wameshinda, tutahakikisha Tanzania bila CCM itawezekana. KANU iliondoka Kenya 2002 na Kenya bado ipo na tunaamini mwafaka wa kitaifa ambapo taifa letu hili lina ombwe la uongozi. Tunatoa rai kwa wale wote ambao wanaona ovu la CCM, wajiunge na UKAWA. Mzee Lowassa historia itakukumbuka kwa ujasiri wako. Wana usalama wanalipa kwa kodi za watanzania wote na sio za CCM, nawaomba wafatilie mchakato huu kwa uadilifu. Tutatumia hekima, umoja wa watanzania na tuwahahakikishia amani, hatutamwaga damu lakini wasituchokoze. Naamini hatua hii tuliofikia, mama Tanzania kwanza, vayama vya siasa baadae.

Mbowe: Leo kwa niaba yangu, viongozi na wanachama wote wa CHADEMA, tumependa kwa dhati kukukaribisha Lowassa na familia yako. Ujio wako umezua hofu kwani hili ni taifa la hofu. Nimesema hofu kwani imeanzia katika chama chako, wamekuwa wakinipigia simu kwa muda mrefu kuwa mnampokea huyo, atawaharibia chama na mimi nikawahahakishia kwa nguvu zote kuwa Lowassa hawezi kuhamia CHADEMA tena nikasema kwa kizungu ‘over my dead body’. Nikajiuliza tangu lini wanaitakia mema CHADEMA, nikajua ni urafiki wa mashaka.

Hofu hii haijaishia kwa CCM bali imeingia hadi CHADEMA, chama hiki ni chetu sote. Chama hiki sio mahakama, simsemi Lowassa ni mtakatifu, nani mmoja wetu humu ndani ni mtakatifu achukue mawe amrushie mwenzake. Taifa hili haliwezi zaidi ya miaka 20, kulipa visasi, kumleta Lowassa katika meza hii haikuwa shughuli nyepesi, tumefanya mashauriano mengi. Eti kwa kuwa tuliwahi kumuita Lowassa mtu mchafu hatuwezi kumkarisha hasa bila ushahidi wa wazi.

Ndo mara ya kwanza mtu aliefikia waziri wa waziri mkuu kuhama CCM, nchi yetu inahitaji mkakati mpya, inahitaji fikra mpya. Watanzania wanataka umoja wetu na hawataki utengano wetu. Eti tutaacha kumpokea Lowassa kiongozi ambae anaungwa mkono na wananchi wengi wa nchi hii, anayeungwa mkono na robo tatu ya wabunge wa ccm. Kama kuna mwanachadema ambae hajatuelewa namuombea kwa Mungu aendelee kumjaza busara. Chama csha siasa ni watu, sasa nimeletewa watu milioni nitawakataa. Siwezi, mtanifukuza uenyekiti na kwa utaratibu huo sitakubali kuondoka.

Kuna wasiwasi kwa watumishi wa umma, Vyombo vya usalama vilivyopo ndio hivyo hivyo vitaendelea, watumishi wa umma ndio haohao wataendelea. Wapo wengine wengi, tutawakaribisha muda ukifika.

Tumebadilisha gia angani ili dynamics ziweze kutekelezeka, CHADEMA kinaongozwa na katiba na hii simwambii Lowassa kwa sababu tayari anayo, nawaambia watanzania wanaotaka kujiunga nasi. Tukiikiua hii tutabamizana. Kwenye chama hiki hatuji kugawana vyeo, niwashukuru sana.

Mwapokee wageni, naombeni msiwaogope wageni kwa kuogopa kuchukuliwa nafasi zenu. Kuna watu tuliwatukana sana, nawaomba na nyie mkija huku muwarushie wa upande wa pili. Tuna imani sana nguvu mpya inayokuja itakua nguvu ya neema. Niwashukuru watanzania wote, tunachopambana nacho sio mtu, tunapambana na mfumo dola. Leo hata ukamchukua malaika ukamshusha CCM na kumuacha kwa mwezi mmoja, ukimchukua tayari atakuwa Ibilisi. Huu ni mpango wa Mungu. Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipotoa shukrani za dhani kwa mtu mmoja wa kipekee sana. Namshukuru sana sana mheshimiwa Kikwete, chama chetu kina idara ya uenezi, hakijafanya kazi nzuri kama aliyofanya Kikwete. Kwa hio mheshimiwa wakati unakatwa Dodoma, wewe unalalamika sisi tunasema yes, mambo haya.

Sio kila linalotokea nia baya, mengine ni mpango wa Mungu. Mungu aliona ili muishi kwa amani na familia yako lazima mtoke CCM ila lazima ujiandae na mazoezi kidogo maana huku kuna mabomu. Waandishi wa habari tunawashukuruni sana, tunaamini ule ushirikiano mliokuwa mnampa team Lowassa mtaweza kutupa.


No comments :

Post a Comment