dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, July 6, 2015

Mola uwape busara CCM


Image result for CCM OF TANZANIA















Wajue ya kwamba chama, muhimu kuliko mtu,
Wasiogope lawama, watetee nchi yetu,
Hakika wanayo dhima wawe wenye uthubutu
Mola uwape busara, Kamati ya CCM.
Mola uwape busara, wajumbe Kamati Kuu,
Watupe amani bora, rais wa mwaka huu,
Wateue wenye dira, wasiwe wenye makuu,
Mola uwape busara, Kamati ya CCM.

Kamati ya CCM, Mola uwape busara,
Yasiwapate magumu, visiwani hata bara,
Wanalo kubwa jukumu, wafanye bila papara,
Mola uwape busara, Kamati ya CCM.

Wajue ya kwamba chama, muhimu kuliko mtu,
Wasiogope lawama, watetee nchi yetu,
Hakika wanayo dhima wawe wenye uthubutu
Mola uwape busara, Kamati ya CCM.

CCM ndiye mama, ni mema malezi yao,
Sio leo tangu zama, umeshinda tetemeko,
Umetuvusha salama, imara chako kivuko,
Mola uwape busara, Kamati ya  CCM

Uwape na ujasiri Yarabi wajumbe wote,
Kikwete ni jemedari, tumaini letu sote,
Upokee ushauri, bila hofu chochote,
Mola uwape busara, Kamati ya CCM.

Kaditama  wajumbe, Kamati ya CCM.
Tafadhali msiyumbe, kazi yenu ni muhimu,
Shikeni huu ujumbe, msije kujilaumu,
Mola uwape busara, Kamati ya CCM.
/Mwananchi.

No comments :

Post a Comment