Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, July 7, 2015

Sitakuwa na kinyongo nikikatwa urais - Balozi Amina Salum Ali.

Balozi Amina Salum Ali.
Mtangaza nia wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Amina Salum Ali (pichani), amesema atakubaliana na matokeo yatakayotolewa na chama chake wakati wa kumteuwa mgombea atakayepeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari visiwani hapa jana, alisema kwa kuwa chama chake leo kinaanza mchakato wa kuchuja majina ya watangaza nia ili kupata mgombea mmoja na kwamba yuko yatari  kupokea matokeo yoyote yatakayotolewa na chama hicho.
Balozi Amina aliongeza kuwa  atahakikisha anamuunga mkono mgombea atakayeteuliwa na chama hicho Jumapili ijayo.



 Alisema bado hajakata tamaa na ana imani kubwa kuwa huenda chama kikamteua yeye kwa sababu sifa na vigezo vyote vinavyohitajika anavyo, hivyo ana kila sababu ya kuteuliwa.
“Naamini chama kitafuata utaratibu tuliojiwekea pamoja na kutenda haki na mimi nitachaguliwa kutokana na vigezo nilivyokuwa navyo ukiwamo uzalendo, uzoefu katika chama na uadilifu,” alisema.
Alisema endapo chama kitampitisha kugombea nafasi hiyo na kushinda, ataunda timu ya watendaji imara kwa ajili ya kuleta mabadiliko yenye wataalamu wa kila aina kutoka pande zote za Muungano bila upendeleo.
“Mimi nikichaguliwa na chama kugombea nafasi hii na wananchi kunipa ridhaa ya kuwa rais wao nitaunda timu iliyobobea katika mambo ya uongozi, taaluma, uzalendo na uadilifu,” alisema.
Alisema Serikali imefanya kazi kubwa katika kuleta maendeleo, lakini bado kuna mengi hayajafanywa na yanahitaji mipango bora ili kuharakisha na kuondoa hali ngumu za wananchi.
Alisema Tanzania ni nchi yenye neema kubwa na chini ya uongozi mzuri kila Mtanzania anaweza kuneemeka kwa neema hizo na yeye anahisi kazi hiyo anaiweza na kuifanya kwa ufanisi mkubwa.
Mwanadiplomasia huyo alisema endapo atapata ridhaa hiyo ya kuteuliwa na chama ya kuwa mgombea wa urais na kupata ushindi katika uchaguzi mkuu, atahakikisha anapambana na ufisadi na kutokomeza vitendo vya udhalilishaji dhidi ya wanawake na watoto.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment