AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, July 5, 2015

Wawili wapigwa risasi wakijiandikisha daftari la kura

Tukio hilo limetokea katika kijiji cha Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja, ambapo watu wasiojulikana waliojifunika nyuso zao waliwapiga risasi watu hao na wengine kuwajeruhi.

Akizungumza na NIPASHE,  mmoja wa majeruhi, Ramadhan Hija Hassan (30), alisema tukio hilo limetokea majira ya saa 4, akiwa na wenzake kwenye doria ya kuangalia watu wasio na sifa ya kujiandikisha kwenye daftari hilo katika kituo cha Nganani Makunduchi.

“Baada ya kuona watoto wadogo ambao hawajafikia umri wa kujiandikisha wakipelekwa vituoni kwa ajili ya kuandikishwa, ndipo tulipoamua kukaa njiani mita 400 kukifikia kituo cha uandikishaji ili kuweza kuwarejesha watoto hao,” alisema majeruhi huyo akiwa hospitalini.

Alisema ghafla lilifika kundi la watu wakiwa wameficha nyuso zao na kuanza kuwapiga kwa kutumia vitu vyenye ncha kali na kuwafyatulia risasi.

Alimtaja mwenzake Kheri Makame kuwa amepigwa risasi ya mguu na kukimbizwa katika hospitali ya Mnazi mmoja.

Alidai kuwa watu hao huenda ni wafuasi wa CCM maarufu kama "Janjaweed" ambao walikuwa na gari nyeupe aina ya Cruizer na Landrover kikosi cha Magereza ambao wote walikuwa na silaha aina ya SMG na vitu vyenye ncha kali.

Ameri Hassan (70), aliyejeruhiwa kwa mawe  kichwani mkazi wa Makunduchi, alisema tokea zoezi la uandikishaji lilipoanza jana, watu hao waliofunika nyuso zao wamekuwa wakiranda katika vituo vya uandikishaji na mitaani.

“Baada ya kuona kijiji chetu kimevamiwa na watu hao ambao ni wageni sio wakazi wa Makunduchi, ndipo tulipoamua kuwafukuza na kuanza kutupiga ambapo tulipambana nao lakini wenzetu walituzidi nguvu na kuanza kufyatua risasi.

Aliwataja majeruhi wengine kuwa ni Khamis Makame Faki, ambaye hadi sasa hajulikani alipo kwani watu hao waliwapiga na kuondoka naye, Amour Pandu Suleiman, aliyejeruhiwa kichwani na yupo chini ya ulinzi wa jeshi la polisi.

Ali Seif Issa (38), mkazi wa Paje mkoa wa Kusini Unguja ambaye amejeruhiwa usoni, mguuni na mgongoni kwa kupigwa viboko, alisema majira ya saa 2 asubuhi akiwa njiani kurudi katika harakati zake, aliona kundi la watu waliojifunika nyuso zao na kuanza kumvamia na kumpiga.

“Nilipojaribu kuwauliza mnanipiga nimefanya nini waliniambia kwa kuwa mimi ni mfuasi wa CUF nawatuma watu wakafanye fujo vituoni. Walinipiga na kuniumiza vibaya kisha kunitupa msituni,”alisema majeruhi huyo.

Daktari wa hospitali ya Al rahma Sheila Mayoya, alisema amepokea majeruhi watano ambao kati yao wawili wamepigwa risasi na walikimbizwa hospitali ya rufaa ya Mnazi Mmoja.

Aidha, majeruhi wengine watatu wamejeruhiwa maeneo mbalimbali ambao wapo katika hospitali hiyo na wanaendelea na matibabu.

Alisema kuwa waliopigwa risasi waliamua kuwapeleka katika hospitali ya rufaa ya Mnazi Mmoja kwa sababu daktari wa mifupa hospitalini hapo amepata dharura.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kusini Unguja Juma Sadi, alisema jeshi la polisi halijapokea taarifa kamili za kujeruhiwa watu hao.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments :

Post a Comment