AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, August 2, 2015

BABIE KABAE : Njia pekee ya kufanikiwa ni kujituma

Babie Kabae

Kwa mara ya kwanza nilikutana na mwanamke huyu visiwani Zanzibar. Ilikuwa mwaka 2010, kwenye onyesho kubwa la mitindo lililoandaliwa na Nguli Mustafa Hassanali.
Onyesho hilo lilifahamika kama ‘Fashion for Health’. Onyesho hili lilifanyika katika Hoteli ya Serena, mimi nilikuwepo kuripoti lakini bi mkubwa huyu licha ya kuwa mwanahabari, siku ile alisimama kama mshereheshaji.
Akiwa amebarikiwa sauti ya kipekee, huku akijiamini aliweza kuendesha onyesho hilo na kutokana na kujiamini kwake aliwateka wafuatiliaji na washabiki na hata kuwafanya wawe na shangwe kila wakati alipokuwa akizungumza.
Namzungumzia Babie Kabae mama wa watoto watatu mwenye asili ya Mombasa nchini Kenya, Mtangazaji wa Redio ya Choice FM.
Kabae ni miongoni mwa wanawake wajasiriliamali wanaokerwa na umasikini wa wanawake. Kimsingi amekuwa akiamini kuwa wanawake hawana sababu hata moja ya kuwa katika hali hiyo.
Kuna fursa nyingi ambazo zikitumika vizuri zinaweza kumtoa mwanamke kutoka kwenye hali moja kwenda kwenye hali nyingine bora zaidi ya maisha.
“Binafsi nimekuwa nikiamini hivyo na kujifunza kutafuta fursa za maendeleo popote pale zilipo lengo hasa ni kwenda mbele”anafafanua mama huyu huku akiachia tabasamu pana kama ilivyo kawaida yake.
Unapoangalia shughuli zake, haitakuchukua muda mrefu kubaini kuwa mama huyu ni ‘Kiraka’. Hii ni kutokana na jinsi anavyopambana kwa kufanya kazi mbalimbali za halali akilenga kuboresha maisha ya familia pato pia kujiingizia kipato.
“Kufanya kazi ni sifa yangu, kufanya kazi kwa ufanisi ndiyo siri ya mafanikio yangu” anaeleza Babie Kabae.
Hivi sasa ukiachilia mbali, utangazaji, ushereheshaji wa sherehe, Babie pia amekuwa ni mjasiriamali wa aina yake.
Amekuwa akifanya kazi kama ofisa uhusiano wa umma, pia ubunifu wa mitindo ya mavazi pamoja na ufugaji wa kuku wa kienyeji.
“Hizi ni kazi zinazoniingizia kipato cha ziada, ufugaji wa kuku huwa naufanya nyumbani kwangu, hili la mitindo nimewaweka mafundi wa kushona maeneo ya kinondoni. Hawa huwa tunasaidiana kutengeneza nguo ambazo huwa naziuza Unguja,” anafafanua.
Safari yake kuja Tanzania
Siku zote hakuna kitu kisichokuwa na mwanzo. Anaanza kwa kusimulia mjasiriamali huyu.
“Safari yangu ya kuja nchini Tanzania, naweza kusema chanzo chake ni Marehemu Rodney Mutie Mengi mwanzilishi wa redio ya East Africa. Ni yeye hasa aliyenihamasisha kuja hapa,” anasema.
“Mutie aliniona kwenye ukurasa wa mbele wa jarida moja la burudani linalotoka nchini Kenya linalofahamika kama PHAT. Lilikuwa ni toleo la kwanza, ambapo kuna mtu alimnunulia na kumuonyesha picha yangu nikiwa na rasta na ndani nikizungumzia muziki ninaoupenda zaidi namaanisha regge,” anafafanua.
Anasema katika kipindi hicho, Redio ya East Africa, 105 FM ilikuwa ikipiga muziki wa rege kwa kiasi kikubwa.
Hivyo alipoisoma habari yake akavutiwa naye na kuamua kumpa nafasi ya kuwa mmoja wa wanafamilia wa Redio East Africa.
“ Kwa kuwa nilikuwa napenda sana kufanya kazi kwenye vyombo vya habari, nilifurahi sana kupata nafasi hiyo. Nikakubali hata kuacha nchi yangu na kila kitu kinachonihusu ili kuja kuanza maisha mapya nchini Tanzania.
Alifanya kazi kwenye kituo hicho cha redio na baadaye televisheni lakini baada ya kukaa hapo kwa muda wa miaka tisa aliamua kuondoka na kurudi tena Kenya.
Kwa nini aliamua kuondoka
Akizungumzia sababu ya kuondoka kwake anasema kuwa, muda wake ulikuwa umefika wa kufanya hivyo, akaona hakuna jinsi ispokuwa kutimiza dhamira yake.
“Baada ya kufanya kazi kwa mafanikio makubwa, niliona wakati umefika wa kupata changamoto mpya. Hivyo nikaona itakuwa vizuri nikitoka na nikafanikiwa kufanya hivyo” Anafafanua.
Alirudi nyumbani Mombasa Kenya na kupumzika muda mrefu kabla ya kupata kazi kwenye kazi ya utangazaji wakati huo, ni kwenye redio moja ya mjini humo.
Kabla ya kwenda kuripoti kwenye kituo chake hicho kipya cha kazi, alipata ujumbe kutoka kwa Mkurugenzi na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Clouds Media, Joseph Kusaga akinitaka kuwa mmoja wa wafanyakazi wake wanaounda timu ya Redio ya Choice FM.
“Nilikubaliana naye na moja kwa moja nikajiunga na timu hiyo ninakofanya kazi hadi hivi sasa”
Aliibukiaje kwenye U-MC?
“Kama nilivyoelezea huko mwanzo kila kitu kina mwanzo wake. Kwangu mimi ushereheshaji meneja wangu alifahamika kama Godfrey Odhiambo Mungu amlaze mahali Pema, ndiye aliyenishawishi kuingia humu,” anafafanua.
Kila siku alikuwa akimwambia kuwa, kutokana na namna alivyokuwa mwongeaji mzuri, anadhani anaweza kuwa Mc mzuri.
Niliamini kuwa nina kipaji hicho, nikaamua kukifanyia kazi, nakumbuka shoo yangu ya kwanza ilikuwa ni katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Mtoto wa Afrika, inayofahamika kama Mama Afrika, inayoandaliwa na mbunifu wa mitindo Ailinda Sawe.
Kitu gani asichokisahau maishani mwake
Vipo vitu vingi lakini kikubwa ni kudhuria mkutano wa US-Africa Commitment na YALI Fellowship Tour.
“Wakati huo mapacha wangu walikuwa na miezi saba tu. Lakini niliweza na nikafanya kazi na vilevile kujifunza vitu vingi. Nilikutana na Rais Barack Obama wakati ule akiwa kwenye kinyang’anyiro cha urais,” anasema na kuongeza “ Nilimpa Rais Obama Kinyago cha Kimasai”.
Wito wake kwa wanawake
Kwanza kabisa nawausia kusoma vitabu. Kila mmoja kwa wakati wake ajaribu kuchukua muda wake kusoma vitabu. Huko atapanua uelewa wake lakini pia uwezo wake wa kuweza kupambanua mambo.
Lakini jambo la pia wasiogope changamoto. Wazichukulie kama daraja la kusonga mbele. Mwisho wafanye kazi kwa bidii. Hii ndiyo njia pekee ya kupambana na umaskini.
“Furaha yangu ni kuona wanawake wote wanajikwamua kiuchumi”.
/Mwananchi.

No comments :

Post a Comment